Wakimbizi 74 wa Burundi warejeshwa kutoka Rwanda

(CRI Online) Machi 13, 2026

Wizara ya Rwanda inayoshughulika na Usimamizi wa Dharura imesema wakimbizi jumla ya 74 wa Burundi wamerejeshwa nyumbani kwa hiari kupitia kituo cha mpakani kilichoko Bugesera nchini Rwanda.

Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X jana Alhamisi, wizara hiyo imesema shughuli hiyo ya kuwarejesha wakimbizi hao nyumbani imewezeshwa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa.

Afisa katika Wizara hiyo amewaambia waandishi wa habari kwamba kundi hilo la wakimbizi linajumuisha watu 62 waliokuwa wakiishi katika Kambi ya Wakimbizi ya Mahama iliyoko Kirehe nchini Rwanda, na wengine 12 kutoka Kigali, mji mkuu wa Rwanda.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha