Bunge la 14 la Umma la China lakamilisha mkutano wa mwaka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2026

Bunge la 14 la Umma la China (NPC) likifanya kikao cha kufungwa kwa mkutano wake wa nne katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Bunge la 14 la Umma la China (NPC) likifanya kikao cha kufungwa kwa mkutano wake wa nne katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Bunge la 14 la Umma la China (NPC), chombo cha utungaji sheria cha kitaifa cha China, limekamilisha mkutano wake wa nne jana Alhamisi katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing la China.

Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wakiwemo Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria kikao cha kufungwa kwa mkutano huo.

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya utendaji wa mkutano huo, aliongoza kikao hicho cha kufungwa kilichohudhuriwa na wajumbe 2,762 wa Bunge la Umma la China.

Wajumbe wa bunge hilo la umma wameidhinisha ripoti ya kazi ya serikali na mwongozo wa maendeleo ya uchumi na jamii wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030).

Wamepitisha Sheria ya Mazingira ya kiikolojia, Sheria ya Uhimizaji wa Umoja na Maendeleo ya Makabila na Sheria ya Mpango wa Maendeleo ya Nchi. Xi Jinping amesaini amri za rais kutangaza sheria hizo.

Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China wameidhinisha ripoti juu ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi ya mwaka 2025 na juu ya muswada wa mpango wa mwaka 2026, na kuidhinisha mpango wa mwaka 2026.

Wameidhinisha ripoti juu ya utekelezaji wa bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa kwa mwaka 2025 na juu ya muswada wa bajeti za serikali kuu na serikali za mitaa kwa mwaka 2026, na kuidhinisha bajeti ya serikali kuu kwa mwaka 2026.

Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma wameidhinisha ripoti za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China.

Pia wamepitisha maamuzi juu ya kuidhinisha ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China kuhusu kazi ya kuzifanyia marekebisho sheria na mapendekezo ya kushughulikia sheria husika na maamuzi husika. Rais Xi amesaini amri ya rais kuhusu maamuzi hayo.

Akihutubia kikao hicho cha kufungwa kwa mkutano wa mwaka, Zhao amesema kwamba mkutano huo wa mwaka umekamilisha utekelezaji wa ajenda zake zote.

Amesema kuwa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano ni kipindi muhimu cha kuimarisha msingi na kusukuma mbele kwa pande zote kazi ya kutimiza kimsingi mambo ya kisasa ya kijamaa ifikapo mwaka 2035, na amesema utekelezaji wenye matokeo mazuri wa mpango huo una umuhimu mkubwa.

Zhao amesisitiza kuwa ni lazima kuweka mkazo katika kusimamia vizuri mambo ya nchi yewenye, na kufanya juhudi za kuanzia mwanzo mzuri na kupiga hatua nzuri ya kwanza kwa utekelezaji wa kazi za kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano.

Kikao cha tume ya utendaji wa mkutano huo wa mwaka, kilichoongozwa na Zhao, kilifanyika kabla ya kikao cha kufungwa kwa mkutano wa mwaka.

Zhao, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, aliongoza kikao cha wenyeviti watendaji kabla ya kikao hicho cha tume ya utendaji wa mkutano wa mwaka.

Kikao cha kufungwa kwa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Zhang Ling)

Kikao cha kufungwa kwa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Zhang Ling)

Zhao Leji akiongoza kikao cha kufungwa kwa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Zhao Leji akiongoza kikao cha kufungwa kwa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya utendaji wa mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) na mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge hilo la Umma, akiongoza kikao cha tatu cha wenyeviti watendaji wa tume hiyo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya utendaji wa  mkutano wa nne wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC), akiongoza kikao cha nne cha tume hiyo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha