Ukame wasababisha watu milioni 3.3 kukabiliwa na njaa nchini Kenya

(CRI Online) Machi 13, 2026

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema kuwa hali ya ukame nchini Kenya inazidi kuwa mbaya ambapo watu zaidi milioni 3.3 katika maeneo kame na nusu-kame wanakabiliwa na njaa.

Shirika hilo limesema katika taarifa yake jana Alhamisi kuwa dharura ya ukame imebadilika kutoka kuwa athari ya tabianchi hadi kuwa msukosuko wa kibinadamu, ukiathiri kaunti 23 kati ya zote 47.

"Watu zaidi milioni 3.3 wako katika uhitaji wa msaada wa chakula, milioni 1.5 kati yao wana uhitaji wa haraka wa maji, na watoto zaidi ya 200,000 wanasumbuliwa na utapiamlo mkali," Shirika hilo limesema, likitoa wito wa kuongezwa kwa maboza ya maji, utoaji wa msaada wa chakula, matibabu dhidi ya utapiamlo, na uungaji mkono wa mifugo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha