Lugha Nyingine
China na Marekani zaanza mazungumzo kuhusu uchumi na biashara mjini Paris

Picha hii iliyopigwa Machi 15, 2026 ikionyesha makao makuu ya Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) mjini Paris, Ufaransa. (Xinhua/Wu Huiwo)
PARIS – Jana Jumapili asubuhi Ujumbe wa China na Ujumbe wa Marekani zilifanya mazungumzo kuhusu masuala ya uchumi na biashara.
Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China alisema katika taarifa yake siku ya Ijumaa kwamba, kutokana na maoni muhimu ya pamoja yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa mkutano wao mjini Busan na mawasiliano yao yote yaliyofanywa kwa njia ya simu, pande hizo mbili zitafanya mashauriano kuhusu masuala ya uchumi na biashara yanayofuatiliwa na pande zote mbili.
Ujumbe wa China unaongozwa na Naibu Waziri Mkuu He Lifeng, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



