Ikulu ya Marekani yapanga kutangaza muungano wa nchi kwa ajili ya kusindikiza meli kupitia Mlango Bahari wa Hormuz

(CRI Online) Machi 16, 2026

Ikulu ya Marekani inapanga kutangaza muungano wa nchi kadhaa zitakazosindikiza meli kupitia Mlango Bahari wa Hormuz.

Ripoti iliyotolewa na jarida la Wall Street jana Jumapili imenukuu maofisa wa Marekani wakisema, mpango huo ambao bado unajadiliwa, unaweza kutangazwa ndani ya wiki hii.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali nyingi hazijatoa ahadi kuhusu jukumu hilo la usindikizaji mpaka mapigano yatakapomalizika kutokana na hatari zilizopo.

Alhamis iliyopita, Kiongozi Mkuu wa Iran Mojtaba Khamenei alitoa wito wa kuendelea kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz na kuahidi kufungua mistari mipya ya mbele katika mapambano ya nchi yake dhidi ya Marekani na Israel.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha