Uchaguzi wa Rais waanza katika Jamhuri ya Kongo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 16, 2026

Wafanyakazi wakithibitisha taarifa za mpiga kura kwenye kituo cha kupigia kura mjini Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Machi 15, 2026. (Xinhua/Zheng Yangzi)

Wafanyakazi wakithibitisha taarifa za mpiga kura kwenye kituo cha kupigia kura mjini Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Machi 15, 2026. (Xinhua/Zheng Yangzi)

BRAZZAVILLE - Wapiga kura zaidi ya milioni tatu waliojiandikisha kupiga kura katika Jamhuri ya Kongo walielekea kwenye vituo vya kupigia kura jana Jumapili kwa ajili ya uchaguzi wa rais nchini humo, huku vituo vya kupigia kura vikifunguliwa kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa saa za Brazaville.

Kwa mujibu wa amri ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Kongo, vituo 6,620 vya kupigia kura viliandaliwa kwenye maeneo mbalimbali 4,011 katika idara 15 zinazounda nchi hiyo.

Wagombea jumla ya saba wanawania kiti cha urais, akiwemo Rais aliyeko madarakani sasa Denis Sassou N'Guesso. Chini ya sheria ya uchaguzi ya nchi hiyo, rais huchaguliwa kwa upigaji kura wa moja kwa moja wa wote katika mfumo wa kupata wingi wa kura kwenye raundi mbili.

Rais huyo aliyeko madarakani sasa Denis Sassou N'Guesso, mwenye umri wa miaka 82, anagombea muhula wa tano mfululizo chini ya bendera ya Presidential Majority, muungano wa kisiasa unaojumuisha vyama vya kisiasa karibia 20.

Wagombea wengine ni pamoja na Joseph Kignoumbi Kia Mboungou, mbunge ambaye pia ni kiongozi wa chama cha "The Chain", ambaye anagombea kwa mara ya tano tangu 2002. Anguios Nganguia Engambe, mkuu wa Chama kwa ajili ya Hatua ya Jamhuri (the Party for Action of the Republic), anagombea kwa mara ya nne mfululizo tangu 2009.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa vyombo vya habari, wakati wagombea sita wanagombea dhidi ya Sassou N'Guesso, upinzani mkuu umegawanyika na haupo kwa kiasi kikubwa, hali ambayo inamfanya kuwa tayari kushinda muhula mwingine wa miaka mitano.

Wajumbe wa uangalizi wa uchaguzi huo kutoka Shirika la Kimataifa la Nchi zinazozungumza Kifaransa na Umoja wa Afrika zimewasili Brazzaville.

Rais aliyeko madarakani sasa Denis Sassou N'Guesso akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura mjini Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Machi 15, 2026. (Xinhua/Zheng Yangzi)

Jamaa akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura mjini Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Machi 15, 2026. (Xinhua/Zheng Yangzi)

Jamaa akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura mjini Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Machi 15, 2026. (Xinhua/Zheng Yangzi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha