Lugha Nyingine
Zambia yapata uungaji mkono wa Benki ya Dunia wa dola milioni 45 za kimarekani kwa ajili ya mpango wa mageuzi
Benki ya Dunia imeidhinisha kutoa dola milioni 45 za kimarekani ili kuunga mkono mpango wa mageuzi ya uchumi wa jumla wa Zambia.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumapili, benki hiyo imesema fedha hizo zilizoidhinishwa chini ya "Mpango wa Pili wa Ufadhili wa Sera ya Maendeleo ya Uhimilivu wa Uchumi na Mabadiliko ya Tabianchi wa Zambia", zinalenga kuunga mkono juhudi za kuimarisha uhimilivu wa kiuchumi wa nchi hiyo.
Fedha hizo zilizoidhinishwa zitaunga mkono ajenda ya mageuzi ya Zambia kupitia sera tatu zinazoingiliana, kila moja ikiwa na msingi wake katika mageuzi maalum ambayo tayari yanatekelezwa na serikali ya nchi hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango wa nchi hiyo Situmbeko Musokotwane amesema, uungaji mkono huo wa bajeti kutoka Benki ya Dunia unaonyesha imani ya jumuiya ya kimataifa inayozidi kuongezeka juu ya ajenda ya mageuzi ya Zambia na dhamira ya serikali katika kuimarisha usimamizi wa kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



