Lugha Nyingine
Rais wa Madagascar ateua waziri mkuu mpya
Rais wa Madagascar Michael Randrianirina amemteua Mamitiana Rajaonarison kuwa waziri mkuu.
Kwenye hafla ya uteuzi iliyofanyika jana Jumapili katika ikulu ya rais, Rais Randrianirina amesema anahitaji "uadilifu" wa Rajaonarison, ambaye amekuwa akifanya kazi kwa muda mrefu katika nyanja ya mapambano dhidi ya ufisadi.
Rais huyo pia amesisitiza kuwa anatarajia waziri mkuu huyo mpya kuunda mara moja serikali itakayopewa jukumu la kutekeleza sera ya ujengaji upya msingi wa kitaifa na kuleta matokeo halisi mapema iwezekanavyo.
Kabla ya uteuzi wake, Rajaonarison alikuwa mkurugenzi mkuu wa Idara ya upelelezi wa mambo ya fedha ya Madagascar, taasisi ya kitaifa inayopambana dhidi ya utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi.
Uteuzi huo unakuja siku sita baada ya Rais Randrianirina kuvunja serikali iliyokuwa ikiongozwa na waziri mkuu wa zamani, Herintsalama Rajaonarivelo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



