Msemaji: China na Marekani ziko katika mawasiliano kuhusu ziara ya Trump

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2026

Beijing – China na Marekani ziko katika mawasiliano kuhusu ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump nchini China, amesema Lin Jian, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China hapa Beijing siku ya Jumatatu.

Msemaji Lin ameyasema hayo kwenye mkutano wa kawaida na waandishi wa habari wakati akijibu swali husika, akiongeza kuwa diplomasia ya viongozi wakuu wa nchi ina jukumu ongozi la kimkakati lisilo na mbadala katika uhusiano wa kati ya China na Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha