Wizara ya Mambo ya Nje: China na Marekani Zaendelea na Mawasiliano Kuhusu Muda wa Ziara ya Rais Trump Nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2026

BEIJING — Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian alipojibu swali kuhusu ripoti za vyombo vya habari zinazosema kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, ameeleza uwezekano wa kuahirisha ziara yake nchini China kutokana na kushughulikia mgogoro na Iran, amesema leo Jumanne kuwa pande zote mbili zinaendelea na mawasiliano kuhusu muda wa ziara hiyo na masuala mengine yanayohusiana. Lin aliongeza kuwa kwa sasa hakuna taarifa zaidi za kutoa.

Kuhusu ripoti zinazosema kuwa "Trump alisema ataahirisha ziara yake kama China haitasaidia kutoa ulinzi wa meli katika Mlango-bahari wa Hormuz," Lin Jian alisema kuwa China imegundua kuwa upande wa Marekani tayari umetoa ufafanuzi kwa umma ambao unakanusha ripoti hizo zisizo za kweli. Marekani imesisitiza kuwa ripoti hizo ni za uongo kabisa na kwamba ziara hiyo haina uhusiano wowote na suala la usalama wa usafiri wa meli katika Mlango-bahari wa Hormuz.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha