Lugha Nyingine
Iran yakana kutafuta kusimamisha vita, yasema vita lazima viishie bila mashambulizi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi akizungumza kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Machi 16, 2026. (Xinhua/Shadati)
TEHRAN - Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi amesema kwamba Tehran haijaomba kusimamisha vita wala mazungumzo na Marekani, akikanusha madai ya Marekani kwamba imeomba suluhu.
Araghchi alitoa ujumbe wake jana Jumatatu kwenye mtandao wa X, akiyataja madai hayo kuwa ni "ya kujidanganya" na akasema vikosi vya Iran vitaendelea kupigana vita hadi Rais wa Marekani Donald Trump atambue kwamba "vita hivyo haramu vilivyolazimishwa kufanywa naye kwa nguvu kwa Wamarekani na Wairan ni vya makosa na havipaswi kurudiwa kamwe."
Araghchi alisema baadaye kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari mjini Tehran, kukomeshwa kwa mgogoro ni lazima kuhakikisha mashambulizi dhidi ya Iran hayatafanywa tena.
"Tunaposema hatutaki kusimamisha vita, si kwasababu tunataka kuendeleza vita," amesema. "Ni kwa sababu vita hivyo ni lazima vimalizike kwa njia ambayo maadui kamwe hawatathubutu kuanzisha tena mashambulizi ."
Araghchi amewashutumu wanaopambana na Iran kwa kujaribu kulazimisha nchi hiyo "kusalimu amri bila masharti" baada ya kuhamasisha uwezo wao kamili.
Ameongeza kuwa mgogoro huo umeendelea kwa zaidi ya wiki mbili, sasa wanaopambana na Iran wako katika kutafuta msaada kutoka nchi ambazo hapo awali waliziona kuwa ni nchi maadui wao na wakitoa wito wa msaada wa kimataifa ili kufanikisha upitaji wa meli kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz. Amesema Iran, inazuia kupita kwa meli za maadui na washirika wao pekee wanaohusika katika mgogoro huo.
Februari 28, Israeli na Marekani zilianzisha kwa pamoja mashambulizi dhidi ya Tehran na miji mingine kadhaa ya Iran, na kumuua Kiongozi Mkuu wa zamani Ali Khamenei, makamanda waandamizi wa jeshi, na raia. Iran ilijibu kwa duru nyingi za mashambulizi ya makombora na droni dhidi ya Israeli na kambi na mali za Marekani katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi akizungumza kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Machi 16, 2026. (Xinhua/Shadati)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi akihudhuria mkutano wa wiki na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Machi 16, 2026. (Xinhua/Shadati)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



