Lugha Nyingine
Thamani iliyoongezwa ya viwanda vya China yaongezeka kwa asilimia 6.3 katika miezi miwili ya kwanza ya 2026

Picha iliyopigwa Machi 16, 2026 ikionyesha mandhari ya Bandari ya Tianjin katika Eneo Jipya la Binhai, Tianjin, kaskazini mwa China. (Picha na Du Penghui/Xinhua)
BEIJING - Thamani iliyoongezwa katika pato la viwanda, ambayo ni kiashiria muhimu cha kiuchumi, imeongezeka kwa asilimia 6.3 kutoka mwaka uliotangulia katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka 2026, takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zilizotolewa jana Jumatatu zinaonesha.
Kwa mujibu wa NBS, kasi hiyo iliongezeka kwa pointi 1.1 za asilimia kuliko kiwango cha Desemba mwaka jana ambapo katika kipindi cha mwezi wa Februari pekee, thamani iliyongezeka ya viwanda ilikua kwa asilimia 0.83 kutoka Januari.
thamani iliyongezeka ya viwanda hutumika kupima shughuli za kampuni kubwa za kiviwanda, kila moja ikiwa na mauzo ya biashara kuu ya angalau yuan milioni 20 (dola za Marekani karibu milioni 2.9).
Mchanganuo wa takwimu hizo unaonyesha kuwa thamani iliyoongezwa ya sekta ya madini liliongezeka kwa asilimia 6.1 kutoka mwaka uliotangulia katika kipindi cha miezi hiyo miwili, huku ile ya sekta ya viwanda likiongezeka kwa asilimia 6.6. Thamani iliyoongezwa ya sekta za uzalishaji na usambazaji wa umeme, joto, gesi, na maji liliongezeka kwa asilimia 4.7.
Msemaji wa NBS, Fu Linghui, ameeleza kuwa ongezeko hilo umesababishwa na kuboreka kwa mahitaji ya ndani, nguvu kubwa ya mauzo ya nje, na matokeo yanayozidi kuwa dhahiri zaidi ya sera za uchumi wa jumla.
“Sekta ya utengenezaji wa zana na vifaa hasa imetoa mchango mkubwa sana katika ukuaji wa jumla wa viwanda,” amesema Fu, akiongeza kuwa katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, thamani iliyoongezwa katika sekta hiyo iliongezeka kwa asilimia 9.3, likichukua asilimia 47.4 ya ukuaji wote.
“Uvumbuzi umebeba jukumu kubwa katika kuongoza maendeleo, huku sekta zinazoibuka zikizidi kusaidia ukuaji wa uzalishaji,” amesema, ambapo thamani iliyoongezwa ya kampuni za viwanda vya teknolojia ya hali ya juu lilikua kwa asilimia 13.1 kutoka mwaka uliotangulia katika kipindi hicho cha Januari-Februari, huku sekta ya viwanda vya bidhaa za kidijitali ikiongezeka kwa asilimia 8.8, zote zikivuka ukuaji wa jumla.
Fu amesema uchumi wa kijani pia umetoa nguvu mpya kwa uboreshaji wa viwanda ambapo katika miezi miwili ya kwanza, uzalishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa upepo uliongezeka kwa asilimia 28.7 kutoka mwaka jana, huku ule wa betri za lithiamu-ion za kuhifadhi nishati ukiongezeka kwa asilimia 84.
Wakati huo huo, Fu ameonya kuhusu athari zinazoendelea za migogoro ya kimataifa ya siasa za kijiografia na hali za nje za kutokuwa na uhakika, huku mahitaji ya ndani yakiwa bado hayaendani na ugavi, uzalishaji wa viwandani bado unakabiliwa na shinikizo kubwa.

Picha iliyopigwa Machi 15, 2026 ikionyesha mandhari ya Gati la Makontena la Longtan kwenye Bandari ya Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Picha na Yang Suping/Xinhua)

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye mstari wa uzalishaji wa kampuni ya zana na vifaa vya kuzalisha umeme kwa upepo katika eneo la maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia, Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Machi 16, 2026. (Picha na Wang Chun/Xinhua)

Picha iliyopigwa Machi 16, 2026 ikionyesha meli ya mafuta ikitia nanga kwenye Bandari ya Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. (Picha na Yu Fangping/Xinhua)

Mfanyakazi akiendesha mashine kwenye karakana katika eneo la maendeleo ya kiuchumi, Jurong, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Machi 16, 2026. (Picha na Zhong Xueman/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



