China yaongeza miji inayoshiriki kwenye kampeni ya majaribio ya kurahisisha biashara ya kuvuka mipaka mwaka 2026

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2026

BEIJING – Mamlaka Kuu ya Forodha ya China (GAC) imetangaza jana Jumatatu kwamba China itaongeza miji yake ya kushiriki kwenye kampeni ya majaribio ya kurahisisha biashara ya kuvuka mipaka hadi kufikia miji 45 katika mwaka 2026, kutoka miji 25 ya mwaka 2025.

Kampeni hiyo ya miezi sita ilianzishwa kwa pamoja na GAC na idara nyingine 23.

Sun Meijun, mkuu wa GAC, ametangaza kwenye mkutano wa kupanga kwamba miji 20 imeongezwa hivi karibuni kwenye orodha hiyo ya kampeni ya majaribio, ikiwa ni pamoja na Hohhot, Changchun, Suzhou, Jinhua, Quanzhou, Nanchang, Yantai, Wuhan, Changsha, Zhuhai, Nanning, Kunming na Xi'an.

Amesema katika kampeni hiyo, hatua mpya zitatolewa mfululizo na kutekelezwa, ambazo zinaweka mkazo katika kuboresha biashara ya bidhaa, kupanua biashara ya huduma, na kuhimiza biashara ya kidijitali na kijani.

Amesema, hatua hizo zitahusisha uvumbuzi katika usimamizi wa forodhani, kuboresha huduma za biashara na nje za aina mpya, kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa wa kuvuka mipaka, kufanya ujenzi wa bandari za kutumia teknolojia za kisasa zaidi, kuimarisha hali ya kufuata pamoja vigezo vya kimataifa, na kutoa uungaji mkono bora zaidi kwa viwanda husika.

Ofisa mmoja wa GAC amesema kurahisisha biashara ya kuvuka mipaka ni muhimu sana kwa kupanua ufunguaji mlango, kuimarisha ushirikiano, na kurahisisha mzunguko wa kiuchumi wa ndani na nje ya nchi, na pia kusaidia viwanda kupata oda, kutafiti masoko na kuongeza faida wakati huu ambapo kuna hali za kutokuwa na uhakika duniani, huku ikionyesha uungaji mkono wa China kwa Mkataba wa Uwezeshaji Biashara wa Shirika la Biashara Duniani na mfumo wa biashara wa pande nyingi.

Tangu mwaka 2018, kila mwaka GAC imekuwa ikiandaa shughuli za kuongeza biashara ya kuvuka mipaka, ikitekeleza hatua 144 kwa jumla ilipofika mwaka 2025, na hatua 110 kati ya hizo zimetekelezwa kote nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha