Ukusanyaji wa Tatu wa Tuzo la Habari za Kimataifa za "Njia ya Hariri" Yaanza Kupokea Kazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2026

Beijing – Shughuli ya ukusanyaji wa tatu wa tuzo ya habari za kimataifa za "Njia ya Hariri" umeanza rasmi jana Machi 16. Tuzo hii zinaandaliwa na Shirikisho la Ushirikiano wa Habari wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRNN) chini ya uratibu wa gazeti la People's Daily, ambalo ni mwenyekiti wa shirikisho hilo.

Tuzo ya habari za kimataifa za “Njia ya Hariri” ni shughuli muhimu ya kichapa ya shirikisho hilo, ikilenga kuendeleza nia za Njia ya Hariri za amani na ushirikiano, ufunguaji na ujumuishi, kujifunzana na kunufaika kwa pande zote. Tuzo hilo linalenga kuhamasisha na kuelekeza mashirika na taasisi za vyombo vya habari kutoka nchi na maeneo yanayohusiana na ujenzi wa“Ukanda Mmoja, Njia Moja” kujifunzana na kusimulia hadithi za pendekezo hilo kwa pamoja.

Tuzo ya tatu ina aina nne: Ripoti Bora, Picha Bora, Video Bora na Ubunifu Bora. Kila aina itakuwa na mshindi mmoja, waliopendekezwa wanne na waliopo kwenye orodha ndefu kumi.

Kazi zinakubaliwa kutoka kote duniani, zote ambazo zinazohusu ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia moja”na zinazoonyesha nia za Njia ya Hariri, mawasiliano ya ustaarabu na kujifunzana, zinazofuata nia ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu, na zenye athari nzuri katika mawasiliano ya kimataifa zinaweza kushiriki kwenye ukusanyaji huo.

Kazi zinazoshiriki lazima ziwe zimemalizika na mashirika ya kigeni pekee au mashirika ya China na kigeni kwa pamoja. Kazi zilizofanywa na mashirika au watu binafsi wa China hazitachukuliwa.

Washiriki wanatakiwa kujisajili na kutuma habari husika za kazi zao kupitia tovuti rasmi (www.brnn.com). Upitishaji wa kazi utafanyika kwa hatua mbili: Upitishaji wa kwanza ni na Kamati ya Kielimu na wa pili ni Kamati ya Majaji. Habari zinazohusu maendeleo ya upitishaji zitatangazwa kwa wakati halisi kwenye tovuti rasmi mtandao huo.

Ukusanyaji wa pili ulifanyika kuanzia Aprili, 2024 hadi Januari 2025, ikipokea kazi karibu 5,000 kutoka nchi na maeneo 110. Kati ya hizo, kazi 58 kutoka nchi 37 zilikuwa washindi.

Shirikisho la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ni jukwaa la ushirikiano lililoundwa na mashirika na taasisi za vyombo vya habari kutoka nchi na maeneo yanayoshiriki katika ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Jukwaa hili linalenga kusaidia vyombo vya habari vya nchi mbalimbali kuimarisha uelewano, kujenga urafiki, kuhizima ushirikiano kupitia utaratibu wa ushirikiano wa kudumu, na kukusanya nguvu ya vyombo vya habari kwa pamoja katika kusimulia hadithi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Hadi sasa, shirikisho hilo limesajiliwa na mashirika 316 ya vyombo vya habari kutoka nchi 117, ikifanya kuwa jukwaa muhimu la ushirikiano wa vyombo vya habari chini ya mfumo wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha