Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Kenya yafikia 71

(CRI Online) Machi 18, 2026

Polisi nchini Kenya imethibitisha kuwa idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko nchini humo imeongezeka hadi kufikia 71.

Katika taarifa yake ya jana Jumanne, polisi imesema zaidi ya nusu ya vifo hivyo vimetokea Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ambako miundombinu mibovu ya mifereji, mito iliyozibwa, na usimamizi dhaifu wa kanuni za ujenzi vimechangia hali hiyo.

“Idadi ya jumla ya vifo vya watu imeongezeka hadi 71, huku vifo vitano vikirekodiwa zaidi. Nairobi inaendelea kuwa ni eneo lililoathiriwa vibaya zaidi, ikiwa na watu 36 waliofariki.” Msemaji wa Jeshi la Polisi la Kenya Michael Muchiri Nyaga amesema katika taarifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha