Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China asema Siasa ya Nguvu ya Kimadaraka Haina Mustakabali
HANOI - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kwamba siasa ya nguvu ya kimadaraka na mabavu ya upande mmoja haviwezi kuungwa mkono na watu na pia havina mustakabali, akitoa wito wa kuimarisha ushirikiano ndani ya mifumo ya pande nyingi ili kulinda amani na utulivu wa bara la Asia.
Jana Jumanne, Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alipomaliza ziara yake nchini Vietnam alisema katika mahojiano na vyombo vya habari vya China, kwamba amani na utulivu wa muda mrefu barani Asia havipatikani kwa urahisi na vinastahili kuthaminiwa na nchi zote.
"Hivi sasa, hali ya kimataifa inapitia mabadiliko makubwa na migogoro ya kikanda inaenea na kufikia katika hali ya kutokudhibitika," amesema Wang, akiongeza kuwa baadhi ya nchi kubwa zinatumia nguvu kwa zipendavyo, na kusababisha tishio kubwa kwa amani na utulivu wa Dunia.
Wang amesema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka mitano ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na ASEAN, mwaka huu na mwaka ujao, China na Vietnam kwa mfululizo zitaandaa Mkutano wa Viongozi wa Uchumi wa APEC, na Vietnam itakuwa nchi mwenyekiti mwenza wa Ushirikiano wa Lancang-Mekong. China, ikiwa ni nguvu muhimu kwa amani, utulivu, na haki duniani, ina nia ya kushirikiana na Vietnam na nchi nyingine katika kuimarisha uratibu na ushirikiano ndani ya mifumo ya pande nyingi kama vile APEC, ASEAN, na Ushirikiano wa Lancang-Mekong ili kulinda maskani yao ya pamoja ya Asia, kusukuma mbele kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya Asia-Pasifiki, na kuweka mfano wa kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Wakati wa ziara yake hiyo nchini Vietnam, Wang alihudhuria mkutano wa kwanza wa mawaziri wa China-Vietnam "3+3" wa mazungumzo ya kimkakati juu ya diplomasia, ulinzi na usalama wa umma, na kuongoza kwa pamoja mkutano wa 17 wa Kamati ya Uongozi wa Ushirikiano wa Pande mbili wa China-Vietnam.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



