Lugha Nyingine
China na Vietnam zafanya mkutano wa kusukuma mbele ushirikiano

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bui Thanh Son mjini Hanoi, Vietnam, Machi 17, 2026. (Xinhua/Hu Jiali)
HANOI - Mkutano wa 17 wa Kamati ya Uongozi wa Ushirikiano wa Pande Mbili wa China na Vietnam umefanyika Hanoi jana Jumanne.
Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bui Thanh Son waliongoza kwa pamoja mkutano huo, na maofisa kutoka wizara mbalimbali na serikali za mikoa ya pande zote mbili wamehudhuria mkutano huo kwa njia ya mtandaoni au kufanya mawasiliano nje ya mkutano.
Wang amesema uratibu mzuri kati ya idara na serikali mbalimbali za mitaa za nchi hizo mbili umepelekea kuboreshwa kwa ushirikiano wa pande zote mbili.
Wang amesema, "Kwa kukabiliwa na hali ngumu yenye utatanishi ya kimataifa, China na Vietnam zinapaswa kuungana mikono ili kusukuma mbele njia ya mambo ya kisasa ya kijamaa, kuanzisha siku hadi siku hali mpya ya uhusiano kati ya vyama na nchi hizo mbili, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kuimarisha hali ya mshikamano na kujitegemea ya nchi za Kusini na kuhimiza amani na utulivu wa kimataifa na kikanda."
Ameongeza kuwa pande zote mbili zinapaswa kupanua wigo wa ushirikiano wa kivitendo, ikiwa ni pamoja na kuhimiza muunganisho wa reli, kuimarisha ushirikiano katika kilimo, umeme, mambo ya fedha, madini muhimu, na uvumbuzi wa kiteknolojia, na kwa pamoja kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi.
Amesema juhudi zinapaswa pia kufanywa ili kudumisha mwelekeo wa mawasiliano kati ya watu, kama vile kuhimiza ushirikiano wa vyombo vya habari, uchapishaji, redio, na filamu, na kuimarisha usimamizi wa hali ya migongano, kusukuma mbele ushirikiano wa baharini, na kukamilisha mapema iwezekanavyo mashauriano kuhusu "Kanuni za Vitendo Kwenye Bahari ya Kusini ya China.”
Kwa upande wake, Son amesema kwamba Vietnam siku zote inaiona China kuwa ni kipaumbele cha juu na chaguo la kimkakati katika sera yake ya mambo ya nje, akiongeza kuwa Vietnam inashikilia kithabiti sera ya kuwepo China moja na inapinga aina yoyote ya shughuli za mafarakano za kuifanya “Taiwan ijitenge".
Ameongeza kuwa Vietnam inakubaliana na China kuhusu hatua zinazofuata za ushirikiano, na ina nia ya kuimarisha zaidi hali ya kuaminiana kimkakati, kujiandaa kwa mawasiliano ya ngazi ya juu, na kuimarisha mawasiliano kati ya vyama na mabunge.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bui Thanh Son wakiongoza kwa pamoja mkutano wa 17 wa Kamati ya Uongozi wa Ushirikiano wa Pande Mbili wa China na Vietnam mjini Hanoi, Vietnam, Machi 17, 2026. (Xinhua/Hu Jiali)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



