Denis Sassou Nguesso achaguliwa tena kuwa rais wa Jamhuri ya Kongo

(CRI Online) Machi 18, 2026

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Kongo imetangaza jana Jumanne kuwa, rais wa sasa wa nchi hiyo Denis Sassou Nguesso amechaguliwa tena kushika wadhifa huo kwa kupata asilimia 94.82 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi uliofanyika Jumapili.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, jumla ya wapiga kura 3,167,909 walisajiliwa, na idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilifikia asilimia 84.64. Wagombea saba walishiriki katika uchaguzi huo, na Uphrem Dave Mafoula amechukua nafasi ya pili kwa kupata asilimia takriban 1.03 ya kura.

Chini ya sheria ya uchaguzi ya nchi hiyo, rais anachaguliwa kupitia upigaji kura wa moja kwa moja, huku mfumo wa duru mbili za uchaguzi kwa wagombea waliopata kura nyingi ukitumika kama hakuna mgombea aliyepata kura nyingi za kumwezesha kushinda moja kwa moja katika duru ya kwanza.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha