Lugha Nyingine
Rais Xi atoa wito wa kuimarisha ushirikiano na Turkmenistan katika sekta za gesi asilia, biashara, na zisizo za maliasili

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Kiongozi wa kitaifa wa watu wa Turkmen na Mwenyekiti wa Baraza la Umma (Halk Maslahaty) la Turkmenistan Gurbanguly Berdimuhamedov, ambaye yuko katika ziara ya kirafiki nchini China, kwenye Jumba la Kuwapokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Machi 18, 2026. (Xinhua/Shen Hong)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano mjini Beijing alipokutana na Kiongozi wa Kitaifa wa Watu wa Turkmen na Mwenyekiti wa Baraza la Umma (Halk Maslahaty) la Turkmenistan Gurbanguly Berdimuhamedov ambaye yuko katika ziara ya kirafiki nchini China, amesema kwamba China na Turkmenistan zinapaswa kupanua ushirikiano katika sekta ya gesi asilia, na kuinua viwango vya biashara na uwekezaji.
Ameongeza kusema kuwa pande hizo mbili zinapaswa kupanua ushirikiano katika sekta zisizo za maliasili, ikiwa ni pamoja na mafungamano ya mawasiliano, kilimo, teknolojia za AI, uchumi wa kidijitali na nishati safi.
Rais Xi amesema, "Mikutano Mikuu Miwili" ya China imefanyika kwa mafanikio siku chache zilizopita, ambapo mwongozo wa Mpango wa 15 wa maendeleo ya uchumi na jamii ya Miaka Mitano (2026-2030) wa China uliidhinishwa.
Pia amesema kwamba utekelezaji wa mwongozo huo utaweka msingi imara kwa China kutimiza kimsingi mambo ya kisasa ya kijamaa, ambayo itanufaisha nchi mbalimbali duniani.
Katika wakati huu wa mwanzoni mwa Mwaka wa Farasi wa jadi wa China, Xi amesema, China inapenda kujadili na Turkmenistan kuhusu ushirikiano, na kunufaika pamoja fursa za maendeleo, ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Turkmenistan yenye mustakabali wa pamoja.
Rais Xi akisisitiza kwamba kuungana mkono ni hali halisi ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Turkmenistan, na bila kujali hali ya kimataifa inabadilika kwa namna gani, China siku zote inaiunga mkono Turkmenistan katika kulinda uhuru, mamlaka ya nchi, na ukamilifu wa ardhi yake. Zaidi ya hayo, Rais Xi amesema China siku zote inaiunga mkono Turkmenistan katika kufuata daima sera ya kutopendelea upande wowote, na China siku zote ni mshirika wa kuaminika kwa Turkmenistan.
Rais Xi amesema, China na Turkmenistan lazima zipambane kithabiti na "nguvu tatu mbaya" za ugaidi, itikadi kali na mafarakano ili kujenga mazingira salama kwa ajili ya maendeleo ya nchi zote mbili.
Kwa upande wake, Berdimuhamedov ametoa pongezi zake kwa China kufanya kwa mafanikio "mikutano mikuu miwili," na amesema mikutano hiyo imetoa maamuzi na mipangilio muhimu kwa ajili ya hatua mbalimbali za maendeleo.
Amesema kuwa ustawi na maendeleo ya China vinanufaisha dunia, na ushirikiano kati ya Turkmenistan na China umekuwa sehemu muhimu ya kuhimiza juhudi katika maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi hizo mbili na unalingana na maslahi ya muda mrefu ya watu wa nchi hizi mbili.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Kiongozi wa Kitaifa wa Watu wa Turkmen na Mwenyekiti wa Baraza la Umma (Halk Maslahaty) la Turkmenistan Gurbanguly Berdimuhamedov, ambaye yuko katika ziara ya kirafiki nchini China, kwenye Jumba la Kuwapokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Machi 18, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais wa China Xi Jinping akifanya matembezi na Kiongozi wa Kitaifa wa Watu wa Turkmen na Mwenyekiti wa Baraza la Umma (Halk Maslahaty) la Turkmenistan Gurbanguly Berdimuhamedov, ambaye yuko katika ziara ya kirafiki nchini China, kwenye Jumba la Kuwapokea Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Machi 18, 2026. (Xinhua/Shen Hong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



