Lugha Nyingine
Ghana yatarajia kutumia teknolojia na uvumbuzi kwa kuongeza uzalishaji wa kilimo

Rais wa Ghana John Dramani Mahama akitoa hotuba kwenye maonyesho ya teknolojia ya kilimo, Accra, Ghana, Machi 17, 2026. (Xinhua/Seth)
ACCRA - Rais wa Ghana John Dramani Mahama amefungua maonyesho ya sayansi na teknolojia ya kilimo siku ya Jumanne wiki hii nchini humo, huku akiahidi uongozi wa serikali katika kutumia teknolojia na uvumbuzi na kuvihimiza kufanya kazi muhimu ili kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuchochea ukuaji tulivu wa uchumi.
Rais huyo amesema, hatua hii ni sehemu moja ya matarajio ya nchi hiyo yanayohusisha kazi nyingi katika kujenga uchumi wa Ghana ulio wa kupata matokeo makubwa zaidi, wa aina nyingi zaidi na wenye hali ya himilivu zaidi. Rais Mahama amesema, serikali inatafuta kujenga uchumi unaotegemea kuongeza thamani, kubadilisha mazao ya kilimo ya Ghana kuwa bidhaa, kusindika zaidi bidhaa zake kwa kuuza nje, kutoa nafasi za ajira zenye heshima kwa watu wake na kutumia bidhaa zilizozalishwa na Ghana.
"Kilimo cha kisasa ni kiini cha matarajio hayo, si kama tu ni sekta finyu kwenye jamii, bali itakuwa injini ya mageuzi ya kiviwanda," amesema.
Rais Mahama amesema kilimo cha kisasa kinahitaji kuendeshwa kwa teknolojia ya kidijitali na uwezo wa wajasiriamali ili kuhakikisha utoaji mkubwa zaidi wa mazao ya kilimo kwa kulisha watu, kutoa malighafi kwa viwanda na kujipatia fedha za kigeni zenye thamani kwa ajili ya uchumi.
Ametoa wito wa kuanzishwa kwa miradi ya kilimo inayoweza kuvutia taasisi za mambo ya fedha na wawekezaji.
Rais huyo amesema kwamba, kuanzia kesho Ijumaa, nchi hiyo itaanza kujenga vituo 60 vya huduma kwa wakulima vinavyolenga kuongeza matumizi ya mashine za kilimo, akiongeza kuwa vituo hivi vitatoa huduma za matrekta, kulima, kusafirisha, mbolea na mabanda ya kusindika nafaka, wakati huohuo kutoa mafunzo na huduma za kutembeza.
Mahama amehimiza vyuo vikuu na taasisi za utafiti kuunga mkono matarajio hayo kwa kuhakikisha miradi yao ya utafiti wa kilimo "inaelekea shambani kutoka maabara, kutoka matokeo ya utafiti hadi uzalishaji, na kuviwezesha viwanda kutumia ujuzi uliopatikana kwa uzalishaji wa bidhaa.”

Mwonyeshaji bidhaa (kulia) akimwelezea mtembeleaji kuhusu bidhaa kwenye maonyesho ya sayansi na teknolojia ya kilimo, Accra, Ghana, Machi 17, 2026. (Xinhua/Seth)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



