Msomi wa Kenya asema mgogoro wa Mashariki ya Kati ni wito wa kuiamsha Afrika kujitegemea kwa nishati

(CRI Online) Machi 19, 2026

Msomi wa sheria na mkurugenzi wa zamani wa mamlaka ya kupambana na rushwa nchini Kenya, Patrick Lumumba amesema, mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati uliotokana na mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, unapaswa kutumika kama wito wa kuziamsha nchi za Afrika kutoa kipaumbele kwa uhuru wa nishati.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua hivi karibuni Lumumba amesema, mgogoro huo unasisitiza haja ya nchi za Afrika kutumia hazina yake kubwa ya mafuta na gesi, hivyo kupunguza utegemezi wa bidhaa za kuagizwa kutoka nje.

Amesema bei za bidhaa za msingi kama chakula, zinaweza kupanda ghafla katika nchi za Afrika zinazotegemea mafuta ya kuagizwa kutoka nje, na hivyo kutatiza juhudi za kudhibiti mfumuko wa bei na kuchochea ukuaji wa uchumi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha