Lugha Nyingine
Wataalamu wa afya wa China watoa elimu ya maji salama Tanzania Zanzibar
Wataalamu wa afya kutoka China, wameandaa warsha kubwa ya kutoa elimu na huduma bila malipo ya kliniki kwa jamii jana Jumatano huko Tanzania Zanzibar ili kueneza elimu ya maji salama.
Tukio hilo, lililoandaliwa na timu ya wataalamu wa China ya kusaidia mradi wa kuzuia na kudhibiti kichocho wa Zanzibar kwa kushirikiana na kundi la 35 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar, lilivutia wakazi wenyeji zaidi ya 300.
Mkuu wa timu hiyo ya wataalam Wang Wei amesema, wakati huu ambapo msimu wa mvua unazidi katika visiwa hivyo, viwango vinavyobadilika vya maji na mafuriko vimeongeza hatari ya maambukizi, hali ambayo imeongeza wasiwasi wa mlipuko wa magonjwa yanayotokana na maji machafu.
Amesema katika kukabiliana na hali hiyo, wataalamu wa afya wa China wamejikita katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu maji salama na hatua za kuzuia magonjwa.
Timu hiyo pia imetoa huduma bila malipo ya kliniki, kufanya vipimo vya magonjwa ya vimelea, na huduma ya kusimamia magonjwa sugu, na hivyo kuwanufaisha mamia ya wakazi wenyeji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



