Lugha Nyingine
Kenya katika tahadhari ya juu ya mvua kubwa
Serikali ya Kenya imesema imepeleka timu za taasisi mbalimbali kuunga mkono operesheni za uokoaji, kusaidia familia zilizoathirika na kurejesha huduma muhimu kabla ya mvua kubwa zinazotarajiwa kuanza leo Ijumaa.
Waziri wa Wizara ya Ndani na Usimamizi wa Maswala ya Kitaifa wa Kenya Onesimus Kipchumba Murkomen katika taarifa yake ya jana Alhamisi ameuhimiza umma kufuatilia ushauri wa Idara ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuwa mvua kubwa zinatarajiwa kuongezeka mwishoni mwa wiki na kuendelea hadi Jumatatu wiki ijayo.
Amesema maofisa wameelekezwa kufanya kazi na maofisa kutoka Jeshi la Polisi na watoa huduma za dharura wengine ili kutoa mwitikio wa haraka na wenye uratibu endapo tukio lolote litatokea.
Murkomen ametoa tahadhari hiyo jana Alhamisi na kusema, idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko ya hivi karibuni imeongezeka hadi kufikia 73, huku watu wengine 7 wakiwa hawajulikani walipo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



