Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wahimiza Iran kuacha mashambulizi, na walaani "sera ya upanuzi" ya Israeli

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2026

Picha iliyopigwa mapema Machi 19, 2026 ikionyesha  ukumbi wa mkutano wa mashauriano wa mawaziri  kuhusu maendeleo ya kikanda, Riyadh, Saudi Arabia. (Xinhua/Wang Haizhou)

Picha iliyopigwa mapema Machi 19, 2026 ikionyesha ukumbi wa mkutano wa mashauriano wa mawaziri kuhusu maendeleo ya kikanda, Riyadh, Saudi Arabia. (Xinhua/Wang Haizhou)

RIYADH - Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 12 za Kiarabu na Kiislamu wamefanya mkutano wa mashauriano wa mawaziri kuhusu maendeleo ya kikanda, ambapo wameihimiza Iran kuacha mashambulizi yake, na wamelaani "sera ya upanuzi" ya Israeli katika eneo hilo.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jana Alhamisi, maofisa wa Bahrain, Misri, Qatar, Saudi Arabia na Lebanon na nchi nyingine wametoa wito kwa Iran kuacha mara moja mashambulizi yake, na pia kusisitiza haja ya lazima ya kuheshimu sheria za kimataifa na kanuni za ujirani mwema, Shirika la Habari la Saudi Arabia limeripoti.

Wamesisitiza kwamba kuacha mashambulizi ni hatua ya kwanza kuelekea kukomesha kupamba moto kwa vita, kufikia usalama na utulivu katika kanda hiyo, na kukomesha msukosuko kwa njia ya kidiplomasia. Pia wameihimiza Iran kuepusha kuchukua hatua yoyote au kutoa tishio lolote vya kufunga au kuzuia usafirishaji wa kimataifa kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz.

Mawaziri hao wamesisitiza kwamba msingi wa uhusiano wa baadaye kati ya nchi mbalimbali na Iran unatokana na kuheshimu mamlaka za nchi na kutoingilia mambo yao ya ndani, kuepusha kushambulia mamlaka ya nchi au ardhi zao na kukwepa kutumia au kuendeleza uwezo wake wa kijeshi kwa kutishia nchi za kikanda.

Mawaziri hao wamesisitiza tena kuunga mkono usalama, utulivu na ukamilifu wa ardhi wa Lebanon, wanatambua mamlaka ya nchi ya Lebanon juu ya ardhi zake zote, na kuunga mkono uamuzi wa serikali ya Lebanon wa kudhibiti silaha ili kuhakikisha zinamilikiwa na serikali.

Pia wamelaani uchokozi wa Israeli dhidi ya Lebanon na "sera yake ya upanuzi" katika eneo hilo.

Mawaziri hao wameahidi kuendelea na mashauriano na uratibu wa kina kuhusu suala hilo, kufuatilia hali inavyoendelea na kutathmini masuala yanayoibuka, na kuhakikisha uwekaji wa misimamo ya pamoja na kuchukua hatua na taratibu muhimu na halali ili kulinda usalama, utulivu na mamlaka ya nchi zao.

Mkutano huo umefanyika katika wakati wa hali wasiwasi inayozidi kuwa mbaya tokea Tarehe 28 Februari, ambapo Marekani na Israeli zilifanya mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran, na Iran na washirika wake wa kikanda walijibu kwa mashambulizi dhidi ya Israeli na maslahi ya Marekani katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati.

Picha iliyopigwa mapema Machi 19, 2026 ikionyesha  ukumbi wa mkutano wa mashauriano wa mawaziri  kuhusu maendeleo ya kikanda, Riyadh, Saudi Arabia. (Xinhua/Wang Haizhou)

Picha iliyopigwa mapema Machi 19, 2026 ikionyesha ukumbi wa mkutano wa mashauriano wa mawaziri kuhusu maendeleo ya kikanda, Riyadh, Saudi Arabia. (Xinhua/Wang Haizhou)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan Al Saud (katikati) akishiriki kwenye mkutano wa mashauriano wa mawaziri  kuhusu maendeleo ya kikanda, Riyadh, Saudi Arabia, mapema Machi 19, 2026. (Xinhua/Wang Haizhou)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha