Ukuaji wa biashara duniani kupungua mwaka 2026 huku kukiwa na shinikizo zaidi kutoka mgogoro wa Mashariki ya Kati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2026

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya ripoti ya hivi karibuni ya Mkadirio ya Biashara na Takwimu Duniani ya WTO kwenye makao makuu yake mjini Geneva, Uswisi, Machi 19, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

GENEVA - Shirika la Biashara Duniani (WTO) limesema Alhamisi kwamba ukuaji wa biashara duniani unatarajiwa kupungua katika mwaka 2026 baada ya ufanisi imara kuliko ilivyotarajiwa mwaka 2025, likionya kwamba mgogoro unaoendelea wa Mashariki ya Kati unaweza kuongeza shinikizo zaidi kwa biashara duniani.

Katika ripoti hii ya hivi karibuni ya Makadirio ya Biashara na Takwimu Duniani, WTO inakadiria kwamba katika hali ya ukuaji wa msingi bila kujumuisha mishtuko ya bei ya nishati, ukuaji wa biashara ya bidhaa duniani utapungua hadi asilimia 1.9 mwaka 2026 kutoka asilimia 4.6 mwaka 2025 kabla ya kurudi katika ukuaji wa asilimia 2.6 mwaka 2027.

Ukuaji wa biashara ya huduma za kibiashara utapungua hadi asilimia 4.8 mwaka 2026, kisha kuendelea kukua tena hadi asilimia 5.1 mwaka 2027, makadirio hayo yanaonyesha. Kwa pamoja, biashara ya bidhaa na huduma itakua kwa asilimia 2.7 katika mwaka 2026 ikilinganishwa na asilimia 4.7 mwaka 2025, ripoti hiyo inasomeka.

Ukuaji wa Pato la Jumla duniani unakadiriwa kupungua kwa kiasi kidogo kutoka asilimia 2.9 katika mwaka 2025 hadi asilimia 2.8 mwaka 2026 na 2027, ripoti hiyo imebainisha.

Hata hivyo, WTO imeonya kwamba makadirio hayo ya msingi yanaweza kuzorota kama mgogoro unaoendelea sasa wa Mashariki ya Kati utaendelea kuvuruga masoko ya nishati.

Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Iran Februari 28, yakivuruga usafirishaji kwa meli duniani, kupelekea bei za mafuta kupanda juu na kutikisa uchumi duniani.

Kama bei ya mafuta ghafi na gesi asilia ya kimiminika itabaki juu katika mwaka mzima wa 2026, ukuaji wa biashara ya bidhaa duniani utapungua kwa asilimia 0.5 hadi asilimia 1.4 tu mwaka 2026. Biashara ya huduma pia itakua kwa kiwango cha chini cha asilimia 4.1. Ukuaji wa Pato la Jumla duniani unaweza kupungua kwa asilimia 0.3, ripoti hiyo imesema.

Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala amesema makadirio huo unaonyesha uhimilivu wa biashara duniani, ikiungwa mkono na biashara ya bidhaa za teknolojia ya hali ya juu na huduma zinazotolewa kidijitali, mabadiliko katika minyororo ya usambazaji na kuepuka kulipizana kisasi kwenye ushuru.

Hata hivyo, Okonjo-Iweala ameonya dhidi ya shinikizo zaidi kutoka kwa mgogoro huo wa Mashariki ya Kati juu ya biashara duniani.

"Ongezeko endelevu katika bei za nishati linaweza kuongeza hatari kwa biashara duniani, huku kukiwa na uwezekano wa kuleta athari kwa usalama wa chakula na shinikizo la gharama kwa watumiaji na kampuni," amesema.

Nembo ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) ikionekana kwenye makao makuu ya WTO mjini Geneva, Uswisi, Machi 19, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

Nembo ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) ikionekana kwenye makao makuu ya WTO mjini Geneva, Uswisi, Machi 19, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

Mkutano na waandishi wa habari juu ya ripoti ya hivi karibuni ya Makadirio ya Biashara na Takwimu Duniani ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) ukifanyika kwenye makao makuu yake mjini Geneva, Uswisi, Machi 19, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

Makao Makuu ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) yakionekana mjini Geneva, Uswisi, Machi 19, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

Makao Makuu ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) yakionekana mjini Geneva, Uswisi, Machi 19, 2026. (Xinhua/Lian Yi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha