Rais Xi atoa salamu za pongezi kwa mkutano wa 10 wa viongozi wa CELAC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 23, 2026

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa salamu za pongezi kwa mkutano wa 10 wa viongozi wa Jumuiya ya Latini Amerika na Karibeani (CELAC), ambao ulifunguliwa Jumamosi huko Bogota, mji mkuu wa Colombia.

Rais Xi amesema kwamba tangu kuanzishwa kwake, CELAC imekuwa ikijitolea kuhimiza amani, utulivu, maendeleo na ustawi katika eneo la Latini Amerika na Karibeani (LAC), na kuingiza msukumo mpya katika mshikamano, ushirikiano na maendeleo ya pamoja ya Nchi za Kusini.

"Mwaka jana, mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China na CELAC ulifanyika kwa mafanikio mwezi Mei mjini Beijing,” Rais Xi amesema, akiongeza kwamba alihudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kutangaza kwamba China na nchi za Latini Amerika zitaanzisha kwa pamoja mipango mikubwa mitano kuhusu mshikamano, maendeleo, ustaarabu, amani na mawasiliano ya kiutamaduni, na mipango hiyo imepata mwitikio mzuri kutoka kwa nchi za Latini Amerika. Amesema, katika mwaka uliopita, China na nchi za Latini Amerika zimeshirikiana kwa karibu, zikisukuma mbele utekelezaji wa hatua madhubuti wa mipango hiyo mitano na kutoa manufaa halisi kwa watu wa pande zote mbili. Rais Xi amesisitiza kwamba China daima itakuwa rafiki mzuri na mshirika mzuri wa nchi Latini Amerika, na itaziunga mkono katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo.

Amesema, China inapenda kushirikiana na nchi za Latini Amerika katika kushikilia usawa na haki za nchi duniani, na kwa pamoja kuandika ukurasa mpya wa kujenga jumuiya ya China na LAC yenye mustakabali wa pamoja.

Colombia kwa sasa ni nchi mwenyekiti wa zamu wa CELAC.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha