Iran yatoa mwongozo wa kanuni za kupita kwenye Mlangobahari wa Hormuz

(CRI Online) Machi 23, 2026

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa jana Jumapili, Machi 22, ikisema Mlangobahari wa Hormuz haujafungwa, ilimradi tu hatua muhimu zilizopitishwa kutokana na hali ya wakati wa vita zifuatwe, meli zinaweza kuendelea kupita kwenye njia hiyo ya maji.

Katika taarifa hiyo, wizara imesema baada ya uchokozi wa kijeshi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran, hali kwenye Ghuba ya Uajemi na Mlangobahari wa Hormuz imekuwa ya hatari, na usalama wa usafirishaji na usafiri wa kikanda umeathiriwa moja kwa moja.

Imesema, ili kutekeleza haki yake halali ya kujilinda, Iran imechukua hatua kadhaa ili kuhakikisha wachokozi hao na waungaji mkono wake hawatumii vibaya Mlangobahari wa Hormuz kuendeleza zaidi malengo yao ya uchokozi.

Taarifa hiyo pia imesisitiza kuwa, ili kurejesha kikamilifu usalama na utulivu endelevu wa Hormuz, uchokozi na vitisho vya kijeshi vya Marekani na Israel dhidi ya Iran lazima vikome, na maslahi halali ya Iran lazima yaheshimiwe kikamilifu.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha