Ethiopia yalenga soko la maua la China chini ya sera ya ushuru-sifuri

(CRI Online) Machi 23, 2026

Ethiopia inalenga kutumia kwa manufaa soko kubwa la maua la China, ikitumia fursa ya sera ya ushuru-sifuri ambayo serikali ya China imetangaza kwa nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China.

Mkurugenzi mkuu wa Jumuiya ya Wazalishaji wa Bidhaa za Maua zinazouzwa nje ya nchi Bw. Tewodros Zewdie, amesema sera hiyo ya ushuru-sifuri ya China itaongeza kwa kiasi kikubwa mauzo ya nje ya bidhaa za maua za Ethiopia na kuimarisha mfumo wake wa biashara kwa ujumla.

Amesema soko la China lina mamilioni ya wateja wa bidhaa zinazotoka Afrika, na ni moja ya mshirika muhimu kwenye sekta hiyo ya maua, hivyo itasaidia kupanua soko la maua na kufungua uwezo wa Ethiopia kikamilfu.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha