Lesotho yapenda kuhimiza ushirikiano kati yake na China

(CRI Online) Machi 23, 2026

Waziri Mkuu wa Lesotho, Sam Matekane, hivi karibuni alipohojiwa na Shirika la Habari la Xinhua, China amesema Lesotho na China zina ushirikiano wa karibu kwa muda mrefu na umepata mafanikio mengi, na kuwa serikali ya Lesotho iko tayari kushirikiana na China kuhimiza ushirikiano wa kuwanufaisha wananchi wao.

Bw. Matekane amesema katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano kati ya Lesotho na China katika sekta za miundombinu, kilimo, elimu umetoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Lesotho, na kuboresha maisha ya wananchi wake.

Bw. Matekane amepongeza sera ya China ya ushuru sifuri kwa nchi za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China, ikiwemo Lesotho. Amesema nguo za Lesotho zinaingia kwenye soko la China, na sera ya ushuru sifuri italeta fursa mpya kwa Lesotho kupanua mauzo ya nje.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha