Maofisa wa Afrika watoa wito wa upatikanaji jumuishi wa maji

(CRI Online) Machi 24, 2026

Maofisa wa nchi za Afrika wametoa wito wa pamoja wa upatikanaji jumuishi na endelevu wa maji kama msingi wa maendeleo ya Afrika, wakisisitiza kuwa kuhakikisha usalama wa maji kwa bara hilo kunaimarisha amani na usalama wa chakula.

Maofisa hao wametoa wito huo kwenye semina ya mtandao ya ngazi ya juu iliyoandaliwa na Umoja wa Afrika (AU) chini ya kaulimbiu 'Maji na Jinsia: Ambako Maji Hutiririka, Usawa Huongezeka' kuhusiana na tukio la kila mwaka la Siku ya Maji Duniani 2026, ikiwaleta pamoja mawaziri, uongozi wa Umoja wa Afrika, na wawakilishi wa wadau wa maendeleo.

Wataalamu na watunga sera wamesema Siku ya Maji Duniani ya mwaka huu, inayoadhimishwa kila mwaka Machi 22, imeunganishwa na uamuzi wa kimkakati wa Umoja wa Afrika wa kufanya usalama wa maji kuwa kipaumbele cha bara la Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha