Lugha Nyingine
Angalau watu 17 wauawa katika mashambulizi ya droni kusini mwa Sudan
Taarifa iliyotolewa na kundi la wanamgambo wa Vikosi vya Uungaji Mkono wa Haraka vya Sudan (RSF) na shuhuda mmoja, inasema angalau watu 17 wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa kwa droni zilizolenga vitongoji vya makazi katika mji wa Lagawa, jimbo la West Kordofan, kusini mwa Sudan.
Kwenye taarifa hiyo iliyotolewa jana Jumatatu RSF imesema mashambulizi hayo yaliyoratibiwa mahsusi dhidi ya hospitali, masoko, na maeneo ya makazi kwenye miji kadhaa katika maeneo ya Kordofan na Darfur, kwa kutumia droni, ni ukiukaji mkubwa na wa wazi wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ambayo inakataza kulenga raia na maeneo ya raia.
RSF imetoa wito wa uchunguzi huru wa kimataifa ili kuwawajibisha waliohusika.
Jeshi la Sudan (SAF) halijatoa maoni yoyote kuhusu tuhuma hizo za kushambulia kwa makombora mji huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



