Lugha Nyingine
Waunda magari wa China wawapita wenzao wa Japan kuongoza mauzo duniani kwa mara ya kwanza
TOKYO – Kampuni za kuunda magari za China zimewapita wenzao wa Japan katika mauzo ya magari duniani kwa mara ya kwanza, na kumaanisha mabadiliko makubwa katika sekta ya magari duniani, kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde ya chombo cha habari cha Nikkei.
Ripoti hiyo imesema kwamba jumla ya mauzo duniani ya kampuni za kuunda magari za Japani ilipungua kidogo hadi magari takriban milioni 25 mwaka 2025, na kusababisha Japan kupoteza nafasi yake ya juu kwa mara ya kwanza ambayo imekuwa ikiishikilia kwa muda mrefu tangu mwaka 2000.
Wakati huo huo, kampuni za kuunda magari za China zimerekodi mauzo ya magari karibu milioni 27 katika mauzo duniani mwaka jana, na kupanda hadi nafasi ya juu duniani kote.
Nikkei imeripoti kwamba, kauli hiyo imetokana na takwimu zilizotolewa na kampuni kubwa za kuunda magari duniani na utafiti uliofanywa na jukwaa la takwimu za magari la MarkLines.
Kati ya kampuni hizo moja moja, BYD imeipiku Ford hadi kuchukua nafasi ya sita duniani mwaka 2025, wakati huohuo kampuni ya Geely imeipiku Honda na kupata nafasi ya nane, ripoti hiyo imesema.
Kampuni sita za kuunda magari za China zimeingia katika nafasi 20 bora duniani, ikiwa ni pamoja na Chery, Changan Automobile, SAIC Motor, na Great Wall Motors, zikizipita tano za Japan. Katika kipengele cha magari yanayotumia umeme, BYD pia imeipiku Tesla na kuwa muuzaji mkuu wa magari ya EV duniani, ripoti hiyo imeongeza.
Tang Jin, mtafiti mwandamizi katika Benki ya Mizuho ya Japan na mtaalamu katika sekta ya magari, amesema kuwa kupanda kwa China hadi kileleni siyo ni mabadiliko rahisi katika uwekaji wa nafasi. Inaashiria marekebisho ya mazingira ya magari duniani, yanayoendeshwa na nguvu za China katika teknolojia ya hali ya juu, ufanisi wa gharama, na utafiti na maendeleo ya haraka.
Ameongeza kuwa Japan inahitaji kutathmini upya mikakati yake katika kuyafanya magari yawe ya kutumia umeme na kujiweka katika nafasi ya soko duniani ili kukabiliana na ushindani unaoendelea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



