Lugha Nyingine
Trump adai kufikiwa kwa "mambo makuu ya makubaliano" na Iran wakati Tehran ikikana mawasiliano yoyote
BEIJING - Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Washington imefikia "mambo makuu ya makubaliano" na Iran na ilikuwa katika mawasiliano na "mtu mkuu," ingawa hata hivyo Tehran imekana mawasiliano yoyote ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja na Marekani.
Trump amewaambia waandishi wa habari jana Jumatatu kwamba pande hizo mbili "zitakwenda kupatana" kwa simu baadaye na kuonya kwamba "itaendelea kupiga mabomu" kama mazungumzo yatashindwa.
Mapema siku hiyo, Trump alisema ameamuru kuahirishwa kwa siku tano kwa mashambulizi yaliyokuwa yamepangwa kwenye mitambo ya umeme na vituo vya nishati vya Iran, akirejelea kile alichokieleza kuwa ni "mazungumzo mazuri sana na yenye tija" katika siku mbili zilizopita yenye lengo la kupunguza mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, Iran imekataa madai hayo. Shirika la habari linalomilikiwa kwa sehemu na serikali ya Iran, Fars limeripoti kwamba hakukuwa na mawasiliano ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja na Trump, huku wizara ya mambo ya nje ya Iran ikisema kauli zake hizo zilikuwa "sehemu ya juhudi za kupunguza bei za nishati na kutenga muda" kwa ajili ya mipango ya kijeshi.
Shirika la habari la Tasnim ambalo nalo linamilikiwa kwa sehemu na serikali ya Iran, likimnukuu afisa mwandamizi wa usalama, limesema Washington imerudi nyuma katika kushambulia miundombinu muhimu baada ya vitisho vya kijeshi vya Iran kuwa vya kuaminika.
Maelezo hayo yanayokinzana yamefuata mabadiliko ya hivi karibuni ya kauli za Trump. Siku chache zilizopita, alisema hakukuwa na "mtu wa kuzungumza naye" baada ya wiki kadhaa za mashambulizi ya Marekani na Israeli ambayo alisema yaliangamiza uongozi wa Iran.
Siku ya Jumamosi, alitoa muda wa mwisho wa saa 48 akiitaka Iran kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, akionya juu ya mashambulizi makubwa, huku Tehran ikiashiria kwamba ingelipiza kisasi katika nchi mbalimbali za eneo hilo kama itashambuliwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



