Jukwaa la Biashara la Kenya na China lajikita katika sera ya ushuru sifuri na kuimarisha uhusiano wa kibiashara

(CRI Online) Machi 24, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Jukwaa la Biashara kati ya Kenya na China limefanyika jana Jumatatu katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, likilenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili chini ya sera ya ushuru-sifuri ya China itakayoanza kutekelezwa Mei Mosi mwaka huu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Rais wa Kenya Kithure Kindiki na Makamu wa Rais wa China Han Zheng ambao waliongoza ujumbe wa maofisa wa ngazi ya juu wa Kenya na China, na wafanyabiashara wakuu na wamiliki wa viwanda kutoka nchi zote mbili.

Kindiki amesema, China ni moja ya nchi zenye nguvu kubwa kiuchumi duniani, ikiwa na zaidi ya watu bilioni 1.4, na kwa Kenya, jambo hilo linawakilisha fursa muhimu katika kuongeza mauzo ya nje, kuimarisha ushirikiano wa kiviwanda, na kuvutia uwekezaji.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa China Han Zheng amesema, China inatarajia kupanua ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Kenya, ambayo ni moja ya washirika wakubwa wa kibiashara katika kanda hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha