Kenya yaandaa jukwaa la biashara ili kuimarisha biashara kati ya China na Kenya

(CRI Online) Machi 24, 2026

Jukwaa la Biashara la China na Kenya limefanyika jana Jumatatu mjini Nairobi, likishirikisha wadau zaidi ya 350 kutoka sekta za serikali na biashara za nchi zote mbili, ili kujadili njia za kuimarisha biashara na uwekezaji wa pande mbili.

Likiwa limejikita kwenye mada kuhusu sera ya China ya ushuru-sifuri kwa nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China, Jukwaa hilo limeandaliwa kwa pamoja na Baraza la China la Kuhimiza Biashara ya Kimataifa (CCPIT) na Shirika la Kuhimiza na Kutangaza Bidhaa Nje la Kenya.

Mwenyekiti wa CCPIT Ren Hongbin amesema, China itatekeleza sera ya ushuru-sifuri kwa nchi 53 za Afrika kuanzia tarehe 1 Mei, ambayo itatoa fursa zaidi kwa wauzaji nje bidhaa wa Afrika kuingia kwenye soko la China.

“Jukwaa hili limeonesha bidhaa za Kenya zinazostahiki kwa sera ya ushuru-sifuri," ameongeza, akitoa wito kwa kampuni za biashara kutoka pande zote mbili kutumia fursa hiyo kuimarisha biashara.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha