Lugha Nyingine
Kampuni za kigeni zawa na matumaini kuhusu fursa chini ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano

Picha ikionesha mandhari ya Mji wa Kimataifa wa Manunuzi Yasiyotozwa Ushuru wa Sanya mjini Sanya, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China. (Picha/People's Daily Online)
China inayofungua mlango ni fursa kwa Dunia. Wakati wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030), China itajenga mifumo mipya kwa uchumi unaofungua mlango kwa kiwango cha juu zaidi, kuendeleza uchumi wa kidijitali, na kutumia kikamilifu AI kuchochea maendeleo ya viwanda yenye sifa bora. Hii si mpango tu wa maendeleo; ni mwongozo wa fursa kwa kampuni za kigeni.
"Ikiwa ni kampuni ya kigeni inayoendeshwa na data, Dun & Bradstreet inafuatilia kwa karibu na inatarajia maendeleo ya kina ya ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa China wakati wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, ukuaji wake thabiti wa uchumi wa kidijitali, na uvumbuzi wake wa kisayansi na kiteknolojia unaoongoza dunia," Wu Guangyu, mkuu wa Dun & Bradstreet Tawi la China, ameiambia People's Daily Online.
Wu amesema tangu kuzinduliwa kwa uendeshaji maalumu wa forodha wa kisiwa kizima katika Bandari ya Biashara Huria ya Hainan (FTP), Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Desemba 2025, kampuni zaidi za China zimekuwa zikijiunga na mtandao wa biashara duniani kwa kutumia namba za utambulisho za Dun & Bradstreet D-U-N-S.
"Likitumia vizuri fursa ya Hainan FTP, Global CHA, jukwaa la habari za kampuni duniani tulilolizindua, limepata matokeo ya kutia moyo, huku watumiaji wake wakizidi 100,000," Wu ameongeza.
Simulizi hiyo ya Dun & Bradstreet inatoa taswira ndogo tu ya jinsi kampuni za kimataifa zinavyopata ukuaji mpya nchini China. Katika miaka ya hivi karibuni, China imerahisisha hatua kwa hatua upatikanaji wa soko kwa wawekezaji wa kigeni, ikiendana kwa bidii na sheria za kimataifa za biashara na uchumi za kiwango cha juu, na kupanua ufunguaji mlango wa kitaasisi.
"Mwanzoni mwa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, China iliweka wazi kujitolea kwake kwa mageuzi ya mfumokazi wa kitaasisi kwa ajili ya kuhimiza uwekezaji wa kigeni na kuunda nguvu bora mpya ili kuvutia uwekezaji wa kigeni, ikionesha mazingira ya biashara yaliyo wazi, ya haki, na yanayotabirika zaidi," Anna An, mkuu wa Henkel Greater China, ameiambia People's Daily Online.
"Tumeshaona ana kwa ana upigaji hatua halisi wa China katika uwezeshaji wa forodha na muunganisho wa miundombinu, ambavyo vimeboresha kwa kiasi kikubwa ufanisi katika uchukuzi wa kuvuka mipaka na kuongeza imani yetu katika kupanua uwepo wetu kwenye soko la China," amesema Wu Dongming, Mkurugenzi Mtendaji wa DHL Express, Tawi la China.
Ufunguaji mlango ni alama ya mambo ya kisasa ya China. Unaonyeshwa katika mfululizo wa hatua halisi: mpango kazi wa kutuliza uwekezaji wa kigeni mwaka 2025, uzinduzi wa uendeshaji maalumu wa forodha wa kisiwa kizima katika Hainan FTP, na toleo la mwaka 2025 la Katalogi ya Viwanda Vilivyohimizwa kwa ajili ya Uwekezaji wa Kigeni.
"Ufunguaji mlango muda wote umekuwa msingi wa kampuni nchini China," amesema Liu Yunfeng, makamu mkuu mtendaji wa Volkswagen Group Tawi la China.
Katika miaka ya hivi karibuni, China imepunguza hatua kwa hatua vizuizi vya uwekezaji wa kigeni na kuimarisha ulinzi wa umiliki wa haki za uvumbuzi kwenye magari yanayotumia nishati mpya na yaliyounganishwa na teknolojia za kisasa za AI. Ufunguaji mlango wa China unasonga mbele hadi ngazi za juu zaidi, na kuunda nafasi kubwa kwa kampuni za kigeni kubeba jukumu kubwa zaidi katika kuendesha uboreshaji wa sekta ya uzalishaji bidhaa na uvumbuzi wa kiviwanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



