Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa UN alaani shambulizi la droni lililoua watu wasiopungua 60 Darfur Mashariki, Sudan
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya watu wasiopungua 60, wakiwemo watoto na wafanyakazi wa afya, katika shambulizi lililofanywa Ijumaa wiki iliyopita kwa droni dhidi ya Hospitali ya Mafunzo ya El-Daein katika jimbo la Darfur Mashariki, Sudan.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, amesema tangu Aprili 2023, Shirika la Afya Duniani limethibitisha kutokea kwa mashambulizi zaidi ya 200 yaliyolenga vituo vya afya nchini Sudan, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 2,000.
Bw. Dujarric amesema Katibu Mkuu amezitaka pande zote kufuata wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ambayo inalinda wafanyakazi wa matibabu na vifaa vyao, na inakataza mashambulizi yanayoelekezwa kwa raia na maeneo ya kiraia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



