IAEA yarudia wito wa kujizuia kwa kiwango cha juu baada ya mashambulizi mapya kwenye kituo cha nyuklia cha Bushehr, Iran

(CRI Online) Machi 25, 2026

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Bw. Rafael Mariano Grossi amerudia wito wake jana Jumanne wa kujizuia kwa kiwango kikubwa kufuatia shambulizi jipya kwenye kituo cha nyuklia cha Bushehr cha Iran.

IAEA imesema kupitia mtandao wa X kwamba imepokea taarifa kutoka Iran kwamba kombora lingine lilipiga kituo hicho siku hiyo ya Jumanne.

Mamlaka za Iran zimesema hakukuwa na uharibifu kwenye kituo hicho, wala majeruhi kwa wafanyakazi wake, na hali ya kituo hicho inaendelea kuwa kawaida.

Bw. Grossi amerudia wito wake wa kujizuia kwa kiwango cha juu, ili kuepuka hatari za usalama wa nyuklia.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha