Lugha Nyingine
Jukwaa la Davos la Majira ya Joto 2026 kufanyika mwishoni mwa Juni

Picha hii iliyopigwa Juni 27, 2024 ikionyesha mwonekano wa nje ya Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Dalian, ukumbi wa Jukwaa la Uchumi Duniani la Majira ya Joto 2024 (2024 Summer Davos) mjini Dalian, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua/Yang Qing)
DALIAN - Jukwaa la Davos la Majira ya Joto 2026 (2026 Summer Davos) litafanyika kuanzia Juni 23 hadi 25 katika mji wa bandari wa Dalian, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, waandaaji wametangaza jana Jumanne.
Jukwaa hilo ambalo pia linajulikana kwa jina la Mkutano wa 17 wa Mwaka wa Mabingwa Wapya wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF), katika mkutano wa mwaka huu, litakutanisha viongozi zaidi ya 1,500 kutoka kwenye sekta za biashara, serikali, asasi za kiraia na wasomi, pamoja na wavumbuzi wa hali ya juu na wanahabari watakusanyika chini ya kaulimbiu ya "Uvumbuzi wa Kiwango Kikubwa."
Washiriki wa mkutano wa jukwaa hilo watajadili zaidi namna gani taasisi zenye nguvu zaidi, mizunguko ya mitaji inayoongezeka na sera zinazotupia macho siku za baadaye vinaweza kubadilisha uvumbuzi na nguvu bora za kiteknolojia kuwa maendeleo ya uchumi, nafasi za ajira na fursa mpya za biashara.
Na ajenda za mkutano wa mwaka huu zitaweka mkazo katika maswali matano muhimu – jinsi ya kustawi katika hali zilivyo sasa za kubadilikabadilika za biashara na viwanda, namna ya kuielewa kipindi kijacho cha mwelekeo wa uchumi wa China, namna gani kuziwezesha teknolojia za kisasa zikite mizizi katika uchumi halisi, namna gani ongezeko la uchumi litaweza kuleta nafasi za ajira na fursa kwa watu wa kizazi kijacho, pamoja na namna gani nishati na mabadiliko ya tabianchi vinaweza kuwa chanzo cha nguvu ya kufanya ushindani.
Waandaaji wa mkutano wamesema kwamba, maswali hayo yanahusiana zaidi kazi za uvumbuzi, ujasiriamali na ushirikiano kati ya viwanda vya kiserikali na kibinafsi na ni muhimu katika kubadilisha changamoto kuwa fursa, na wakati huohuo kuchochea sera na mbinu mpya kwa kuhimiza ongezeko la uchumi.
Wamesema maandalizi husika ya mkutano wa jukwaa hilo yanaendelea kwa sasa.
Jukwaa hilo la Davos la Majira ya joto lililoanzishwa na WEF mwaka 2007, mkutano wake unafanyika kila mwaka nchini China, na miji miwili ya bandari ya Tianjin na Dalian inaandaa mkutano kwa zamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



