AU yamteua rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwa mwakilishi mkuu wa Pembe ya Afrika, Bahari Nyekundu

(CRI Online) Machi 26, 2026

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf amemteua Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwa Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Afrika kwenye eneo la Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu.

Katika taarifa ya kamisheni hiyo iliyotolewa jana Jumatano, AU imesema, akiwa Mwakilishi Mkuu wa AU kwa Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu, jukumu la Bw. Kikwete limeelezwa kuwa litajumuisha, kusukuma mbele diplomasia ya kuepusha migogoro kabla haijatokea, kuwezesha mazungumzo jumuishi ya kisiasa, kuhimiza kujenga imani miongoni mwa wadau, na kuimarisha mifumo ya ushirikiano wa kikanda, inayolenga kuhimiza amani na utulivu endelevu.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha