Makamu wa Rais wa China akutana na Rais Kenya Ruto

(CRI Online) Machi 26, 2026

Makamu wa Rais wa China Han Zheng ambaye alikuwa ziarani nchini Kenya kuanzia Machi 22 hadi 25, alikutana na kufanya mazungumzo na Rais William Ruto wa Kenya mjini Nairobi juzi Jumanne, Machi 25.

Kwenye mazungumzo yao Bw. Han Zheng ameeleza kuwa, China inapenda kushirikiana na Kenya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, vilevile matokeo ya mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika(FOCAC)uliofanyika mjini Beijing, ili kuingiza msukumo mpya katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili, na kutoa mfano mzuri katika kujenga Jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Rais Ruto amesema Kenya iko tayari kutumia fursa ya utekelezaji wa sera ya ushuru-sifuri kwa Afrika kuimarisha uratibu wa mikakati ya maendeleo na China, kupanua ushirikiano katika sekta zote ili kunufaishana.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha