Lugha Nyingine
China yasema jambo la muhimu zaidi kwa sasa ni kusimamisha mapigano Mashariki ya Kati
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian, amesema huku athari zinazosambaa za mgogoro zikileta pigo kwa amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati na kwingineko, jambo la muhimu zaidi kwa sasa ni kusimamisha mapigano na kumaliza uhasama.
Akijibu swali kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatano, Lin amesema mazungumzo ni njia ya kukwamua hali hiyo, na China itaendelea kuonesha umuhimu wa kiujenzi katika kuhimiza amani na kusimamisha vita.
Bw. Lin amesema, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi alipofanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Iran, alieleza msimamo wa China kuwa masuala yote ya kikanda yanapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na si kupitia matumizi ya nguvu ya kijeshi.
Amesema kufanya mazungumzo ni vizuri kuliko kuendelea na mapigano, na China inatoa wito kwa pande mbalimbali kutumia fursa zote za amani na kuanza mchakato wa mazungumzo mapema iwezekanavyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



