Lugha Nyingine
Kutoka kwenye udongo hadi kuwa data: Namna teknolojia inavyowezesha kilimo cha kisasa cha China

Mwanasayansi mwandamizi wa kilimo Yan Ji akikagua ukuaji wa mboga za majani kwenye kituo cha sayansi na teknolojia za siku za baadaye za kilimo katika eneo la kielelezo la kilimo, Changji, Mkoa wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Februari 10, 2025. (Xinhua/Ding Lei)
Je mashamba ya siku za baadaye yatakuwa na mwonekano gani?
Kwenye mashamba, droni hupita angani kote kwa mpangilio mzuri. Ndani ya mabanda ya kilimo cha kisasa cha kijani, roboti za ukaguzi huteleza kimya kimya kwenye mistari, vitambuzi vyao vikichunguza majani na mashina kama yana dalili za ugonjwa. Chini ya udongo, vichunguzi vya kidijitali vinafuatilia unyevu na virutubisho, vikisambaza data kwa wakati halisi.
Kwenye chumba cha karibu cha udhibiti, skrini kubwa huonesha namba - joto, unyevunyevu, uoevu wa udongo na mwanga wa jua. Algorithimu huchambua data na kutuma maelekezo mara moja kupitia mitandao ya 5G, ikiamsha mifumo ya umwagiliaji na vifaa vya kuweka mbolea kote shambani.
Kile ambacho hapo awali kilionekana kuwa ni simulizi kutoka hadithi za kubuniwa za tayari kinatokea kwenye kijiji cha Tianjiaying katika wilaya ya Nanzhang, mji wa Xiangyang, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China.

Mfanyakazi akiendesha mfumo wa kiotomatiki wa AI wa kupanda mbegu kwenye Shamba la Youyi chini ya kampuni ya Kundi la Beidahuang katika Mji wa Shuangyashan, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Wang Song)
Katika eneo maalum la viwanda vya kisasa vya kilimo la kijiji hicho, mabanda 82 ya kilimo cha kisasa cha kijani hufanya kazi chini ya mfumo wa usimamizi wa kidijitali ambao unaunganisha teknolojia za udhibiti wa hali ya joto, umwagiliaji na ufuatiliaji katika jukwaa moja jumuishi. Wakulima wanaweza kurekebisha uingiaji hewa, umwagiliaji na uwekaji mbolea kupitia simu zao za mkononi huku mashine za kiotomatiki zikishughulikia sehemu kubwa ya kazi za shambani.
"Kwa mfumo huu, mtu mmoja anaweza kusimamia kutokea mbali mamia ya mabanda ya kilimo cha kisasa cha kijani, na kupunguza gharama za wafanyakazi kwa kiasi kikubwa wakati huohuo ikiongeza mavuno kwa zaidi ya asilimia 50," amesema Su Wei, mkurugenzi wa Kituo cha Uvumbuzi kwenye Eneo la Tianjiaying la Kampuni ya Teknolojia ya Jinmeikelin, Tawi la Hubei.
Mabadiliko hayo yanayotokea Tianjiaying ni sehemu ya mabadiliko mapana yanayotokea kote China, ambapo teknolojia za kidijitali zinabadilisha kwa kasi kubwa kilimo.
Ukuaji wa teknolojia za namna hiyo unachochea sekta hiyo inayopanuka kwa kasi. Takwimu zinaonyesha kuwa soko la kilimo cha teknolojia za kisasa (smart agriculture) la China limekua kutoka thamani ya Yuan bilioni 38.8 (Dola za Marekani Bilioni 5.63) katika mwaka 2017 hadi Yuan takriban bilioni 100 mwaka 2024, huku kiwango cha ukuaji wa mwaka kikiwa cha asilimia takriban 15.
Wakati wa "mikutano mikuu miwili" ya China ya mwaka huu, watunga sera na wataalamu wamesisitiza kilimo cha teknolojia za kisasa ni kichocheo muhimu cha kukifanya kilimo kuwa cha kisasa.
Zaidi ya kuongeza tija, teknolojia hizo pia zinaleta manufaa halisi kwa jamii za vijijini.
Kwa mfano, eneo maalum la kilimo cha teknolojia za kisasa katika wilaya ya Nanzhang limenufaisha jamii za wenyeji kwa kushirikisha kaya zaidi ya 300 kwenye kilimo cha kisasa. Kwa kuwa na mavuno mengi, mazao mbalimbali na njia thabiti za mauzo, wakulima wanapata fedha zaidi huku wakifanya kazi karibu na nyumbani.
Ndani ya moja ya mabanda ya kilimo cha kisasa cha kijani chenye joto vuguvugu, mwanakijiji Yang Shuhui mwenye umri wa miaka 60 alikuwa akitembea polepole kwenye mistari, akichuma nyanya zilizoiva na kuziweka kwenye kapu.
"Ni rahisi sana kufanya kazi hapa, na ninaweza kupata yuan 2,000 hadi 3,000 kwa mwezi karibu na nyumbani," amesema.

Fundi akikagua ukuaji wa miche kwenye kituo cha miche chenye kutumia AI katika Kijiji cha Shuangxing cha Eneo la Yongchuan, Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Huang Wei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



