Ikulu ya White House yatishia mashambulizi makali dhidi ya Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 26, 2026

Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, Washington, D.C., Marekani, Machi 25, 2026. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)

Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, Washington, D.C., Marekani, Machi 25, 2026. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)

WASHINGTON - Msemaji wa Ikulu ya Marekani ya White House Karoline Leavitt amesema, Rais wa Marekani Donald Trump "atafungua kuzimu (unleash hell)" kama Iran itakataa kufikia makubaliano juu ya vita vinavyoendelea vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

"Rais Trump hadanganyi na yuko tayari kufungua kuzimu," amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Ikulu ya White House jana Jumatano. "Ghasia zozote zaidi," amesema, itakuwa ni kwasababu Iran "imekataa kuelewa kuwa tayari wameshashindwa na kukataa kufikia makubaliano."

Leavitt amekataa kubainisha ni nani Washington inajadiliana naye juu ya jinsi ya kumaliza vita hivyo na Iran.

"Hatutaeleza kwa kina majadiliano na mazungumzo haya ambayo yanaendelea kufanyika kwani, bila shaka, unaweza kufikiria, haya ni majadiliano nyeti sana ya kidiplomasia," amesema.

Leavitt amedai vita hivyo, vilivyoanza Februari 28, bado viko njiani kuendelea kwa wiki nne hadi sita.

"Hakuna mazungumzo au majadiliano kati ya Iran na Marekani," amesema msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghaei kwenye mahojiano maalum na Chombo cha Habari cha India Today siku hiyo ya Jumatano.

"Hakuna mtu anayeweza kuamini diplomasia ya Marekani," Baghaei amesema, akibainisha kuwa Iran ilijionea mambo mabaya sana katika diplomasia na Marekani, yaliyothibitishwa na mashambulizi ya Marekani wakati wa mazungumzo kuhusu suala la nyuklia siku za nyuma.

Ebrahim Zolfaghari, msemaji wa kamandi kuu ya kijeshi ya Iran, Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya, amesema Marekani inajadiliana na yenyewe peke yake kutokana na mzozo wake wa ndani.

Ameitaka Marekani kuacha kuficha kushindwa kwake kwa kuita ni "makubaliano," akiongeza, "nguvu ya kimkakati ambayo maadui walikuwa wakijisifu nayo imegeuka kuwa kushindwa kimkakati."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha