Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri aipongeza China kwa kazi yake ya kiujenzi katika kukabiliana na changamoto za Mashariki ya Kati
CAIRO - Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty amesifu uhusiano "bora na wa kirafiki sana" kati ya Misri na China, akisisitiza kazi ya kiujenzi ya Beijing katika kukabiliana na changamoto za Mashariki ya Kati.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri jana Jumatatu katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala, Abdelatty amesisitiza "sera za kuhimiza juhudi, zenye uwiano, na busara" za China katika eneo hilo.
"Tuna maoni na malengo sawa ya kuhimiza mazungumzo na njia ya kidiplomasia ili kutatua matatizo yaliyopo, kwa sababu vita vinaweza tu kusababisha uharibifu," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.
Mapema Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Abdelatty kujadili hali katika eneo la Mashariki ya Kati, na waziri huyo wa Misri ameyaelezea mazungumzo hayo kuwa ni "ya kichangamfu na ya kiujenzi."
Abdelatty ameuelezea uhusiano wa pande mbili kuwa ni wa muhimu na unaoendelea kwa hatua madhubuti, na amesema kuwa nchi hizo mbili zinadumisha mawasiliano ya kila baada ya muda uliowekwa kwenye ngazi ya juu.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Abdelatty alielezea juhudi kubwa za kidiplomasia za Misri, zilizofanywa chini ya mwongozo wa uongozi wa nchi hiyo na kwa uratibu na washirika wa kikanda na kimataifa, ili kuzuia hali wasiwasi ya kupamba moto kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ambao umeathiri usalama wa nchi kadhaa za Kiarabu.
Amesisitiza tena dhamira ya Misri katika kufuata njia ya kidiplomasia na kuhimiza mazungumzo.
Israeli na Marekani zilianzisha mashambulizi kwa pamoja dhidi ya Tehran na miji mingine kadhaa ya Iran Februari 28, ambapo Kiongozi Mkuu wa wakati huo wa Iran Ali Khamenei, makamanda waandamizi wa jeshi, na raia waliuawa katika mashambulizi hayo. Iran ilijibu kupitia mashambulizi mfululizo ya makombora na droni dhidi ya Israeli na kambi na mali za Marekani katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati.
Jumatatu wiki hii, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba Washington na Tehran zinatafuta makubaliano na zinafikia kauli moja katika "mambo muhimu " baada ya yeye kuamuru kuahirisha kwa siku tano mashambulizi yaliyokuwa yamepangwa dhidi ya majengo ya kuzalisha umeme na miundombinu ya nishati ya Iran.
Jana Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi alisema kwamba Iran na Marekani zimebadilishana ujumbe mbalimbali kupitia wapatanishi katika siku chache zilizopita, lakini Tehran haijafanya mazungumzo yoyote na Washington tokea Februari 28.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



