Lugha Nyingine
China kufungua majengo 10 makuu ya utafiti wa kisayansi kwa watafiti wa kimataifa mwaka 2026

Picha hii iliyopigwa Januari 15, 2025 ikionyesha jengo la utafiti wa muunganisho wa nyuklia, ambalo ni jengo la kufanya majaribio la Experimental Advanced Superconducting Tokamak (EAST), huko Hefei, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. (Xinhua/Huang Bohan)
BEIJING - China itawafungulia watafiti wa kimataifa majengo 10 makuu ya utafiti wa kisayansi mwaka huu, habari ilitangazwa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Zhongguancun (Jukwaa la ZGC) 2026 uliofanyika Beijing jana Jumatano.
Majengo hayo yatahusu baadhi ya majukwaa ya utafiti wa kisayansi ya hali ya juu zaidi nchini China, yakiwemo Aperture Spherical Radio Telescope (FAST) ya mita mia tano iliyoko Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China, Miundombinu ya Mfano na Utafiti wa Mazingira ya Anga ya Juu katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, na Jengo la Majaribio la Experimental Advanced Superconducting Tokamak katika Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China.
Tangazo hilo limeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kusukuma mbele zaidi Mpango Utendaji wa Ushirikiano wa Kisayansi wa Kimataifa ulio wa kufungua mlango, ambao ni mradi ulioanzishwa na China na washirika wa kimataifa mwaka 2025 ili kujenga mazingira ya kimataifa yaliyo wazi, ya haki, sawa na yasiyobagua kwa ajili ya maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia.
China inahimiza uvumbuzi wake wa kiteknolojia kwa kupitia ushirikiano wa kimataifa wa kiwango cha juu. Mwongozo wa Mpango wake wa 15 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii wa Miaka Mitano (2026-2030) uliotolewa mapema mwezi huu, umeamua kujenga mfumo wa kiikolojia ulio wa kufungua mlango na wa uvumbuzi wenye nguvu ya kufanya ushindani duniani, na kuunga mkono juhudi za pamoja za wanasayansi wa kote duniani ili kukabiliana na changamoto za kisayansi zilizo za kimsingi na za kimaendeleo zaidi na kuelekea zaidi siku za baadaye.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



