Watu 28 wauawa, 29 wajeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa kwa droni katikati na magharibi mwa Sudan

(CRI Online) Machi 27, 2026

Watu 28 wameuawa na wengine 29 wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili yaliyofanywa Jumatano kwa droni yakilenga miji miwili ya katikati na magharibi mwa Sudan.

Vyanzo vya habari katika eneo hilo vimesema droni ilishambulia soko kuu katika mji wa Saraf Omra katika Jimbo la Darfur Kaskazini mapema Jumatano, pamoja na maeneo mengine mawili, na kuua watu 22 na kujeruhi wengine 17.

Katika taarifa yake ya siku hiyo Jumatano, jeshi la Vikosi vya Uungaji Mkono wa Haraka (RSF) limelituhumu Jeshi la Sudan (SAF) kufanya shambulizi hilo, ambalo imelielezea kuwa ni sehemu ya “operesheni za kurusha makombora zilizoratibiwa mahsusi dhidi ya raia.”

Jeshi la Sudan halijatoa maoni yoyote kuhusu tuhuma hizo.

Kwenye tukio lingine katika mji wa Al-Rahad katika Jimbo la Kordofan Kaskazini, mashuhuda wameripoti kuwa watu sita waliuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa kwa droni lililolenga gari la abiria lililokuwa likielekea katika mji wa Um Rawaba.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha