Lugha Nyingine
Makamu Rais wa China akutana na Rais wa Afrika Kusini juu ya uhusiano wa pande mbili

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Cape Town, Afrika Kusini, Machi 25, 2026. (Xinhua/Liu Bin)
CAPE TOWN - Makamu Rais wa China Han Zheng amekutana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mjini Cape Town, Afrika Kusini Jumatano wiki hii, huku pande zote mbili zikiahidi kuongeza kwa kina ushirikiano na uhusiano wa pande mbili.
Han amewasilisha salamu za urafiki na za kutakia kila la kheri za Rais wa China Xi Jinping kwa Rais Ramaphosa. Wakati wa ziara yake hiyo, Han na mwenzake wa Afrika Kusini Paul Mashatile wataongoza kwa pamoja mkutano wa tisa wa wajumbe wote wa Kamisheni ya Mataifa Mawili ya China na Afrika Kusini.
Han amesema, chini ya mwongozo wa maafikiano muhimu yaliyofikiwa kati ya Marais Xi na Ramaphosa, watakumbuka kwa pande zote mafanikio ya ushirikiano katika maeneo muhimu kati ya nchi hizo mbili na kupanga kwa mpangilio mzuri mwelekeo na majukumu muhimu kwa hatua inayofuata.
Han amebainisha kuwa China inaweka umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wake na Afrika Kusini na iko tayari kushirikiana na nchi hiyo ili kusukuma mbele zaidi ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika Kusini katika zama mpya ulioanzishwa na viongozi hao wawili wa nchi.
Amesema, Rais Xi hivi karibuni alitangaza kwamba kuanzia Mei 1, China itatekeleza kikamilifu hatua za ushuru-sifuri kwa nchi 53 za Afrika ambazo imeanzisha uhusiano wa kidiplomasia nazo. Katika muktadha huo, Han amesema, China ina nia ya kushirikiana na Afrika Kusini ili kukamilisha, mapema iwezekanavyo, mipango ya mavuno ya mapema chini ya Mfumo wa Makubaliano juu ya Ushirikiano wa Kiuchumi kwa Maendeleo ya Pamoja ili kuhakikisha kwamba Afrika Kusini inaweza kufaidika kwa msingi wa muda mrefu na tulivu kutokana na hatua hizo za ushuru-sifuri za China.
Kwa upande wake, Rais Ramaphosa amemwomba Han kuwasilisha salamu zake za dhati na za kutakia kila la kheri kwa Rais Xi.
Ramaphosa amesema kwamba Afrika Kusini inafuata sera ya kuwepo kwa China moja. Amebainisha kuwa ushirikiano kati ya Afrika Kusini na China ni wa kipekee na wa kimkakati, ambao unaelekea maendeleo, na kukuza kwa ufanisi maendeleo na upigaji hatua wa Afrika Kusini na Afrika.
Rais Ramaphosa ameelezea shukrani kwa Rais Xi kwa kutangaza utekelezaji huo kamili wa hatua za ushuru-sifuri, akisema kwamba Afrika Kusini itatumia vema sera hizo kupanua mauzo ya nje kwenda China na kuimarisha ushirikiano na China katika maeneo kama vile miundombinu, uwekezaji na teknolojia, ili kuimarisha zaidi uhusiano wa pande mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



