Lugha Nyingine
Mkutano wa 14 wa mawaziri wa WTO wafunguliwa Cameroon huku ukitoa wito wa mageuzi ya haraka

Wajumbe wakihudhuria Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Yaounde, Cameroon, Machi 26, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)
YAOUNDE - Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) wa siku nne umefunguliwa jana Alhamisi huko Yaounde, Cameroon, ambapo mawaziri wa uchumi, biashara, na maendeleo kutoka nchi mbalimbali duniani, pamoja na wajumbe wa mashirika ya uchumi na biashara duniani wamehudhuria mkutano.
Katika hotuba yake ya makaribisho, Waziri wa Biashara wa Cameroon Luc Magloire Mbarga Atangana amesisitiza dhamira ya nchi hiyo katika kuhimiza biashara iliyo ya usawa, ufunguaji mlango, na jumuishi.
"Moja ya malengo makuu ya mkutano huu ni kupiga hatua katika mpango wa mageuzi unaolenga kuimarisha uwezo wa WTO wa kukabiliana na uchumi wa dunia unaobadilika. Mageuzi lazima yalifanye shirika la WTO liwe na nguvu na ufanisi zaidi," amesema, akisisitiza hitaji la mageuzi ya WTO.
Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala amezungumzia changamoto zinazoikabili biashara duniani, akibainisha migogoro katika Mashariki ya Kati, Sudan, Ukraine, na kwingineko kuwa ni sababu za kuleta vurugu na hali ya kutokuwa na uhakika. Amezihimiza nchi wanachama mbalimbali zijitahidi kuanzisha njia ya kusonga mbele kwa ajili ya mfumo wa biashara duniani.
"Hakuna shaka lolote kwamba mfumo wa biashara duniani unakabiliwa na mvurugiko mbaya zaidi katika miaka 80 iliyopita," Okonjo-Iweala amesema. "Ni wakati wa kushughulikia matatizo yanayolikumba shirika hilo na kuathiri utendaji wake. Hatuwezi kulalamika kila mara kisha kukosa fursa ya kuondoa matatizo."
Mkutano huo wa mawaziri, ambao ni chombo cha juu zaidi cha kufanya maamuzi cha WTO, katika hali ya kawaida, mkutano huo unafanyika kila baada ya miaka miwili.

Wajumbe wakihudhuria Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Yaounde, Cameroon, Machi 26, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



