Jukwaa la uchumi la Asia latoa wito wa kuimarisha ushirikiano na mfumo wa pande nyingi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2026

Roboti ikionekana kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia (BFA) 2026 katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Machi 25, 2026. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

Roboti ikionekana kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia (BFA) 2026 katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Machi 25, 2026. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

BOAO, China – Huku ongezeko kubwa la ushuru lililotokana na uamuzi wa upande mmoja na kujihami likichochea hali ya kutokuwa na uhakika duniani, washiriki kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026 wametoa wito wa ushirikiano wa kina zaidi wa kikanda na mfumo imara zaidi wa biashara wa pande nyingi ili kukabiliana na changamoto zilizopo na kuimarisha msingi wa ukuaji duniani.

Wong Kan Seng, naibu waziri mkuu wa zamani wa Singapore, amebainisha kuwa hatua kubwa za ushuru zimepeleka mawimbi ya mshtuko kote duniani.

"Ushuru huu umemomonyoa hali ya kutabirika kwa mazingira ya uendeshaji, kutatiza mipango ya muda mrefu, na kudhoofisha kuaminiana na kushirikiana," Wong amesema, akiongeza kuwa nchi zinalazimika kutathmini upya washirika wao wa kibiashara, mbinu za biashara, na hatari tarajiwa ambazo zitakabiliana nazo.

"Kustawisha APEC: Kukabiliana na Changamoto na Kuchangia Fursa Pamoja" katika Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Asia la Boao (BFA) 2025, Boao, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

"Kustawisha APEC: Kukabiliana na Changamoto na Kuchangia Fursa Pamoja" katika Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Asia la Boao (BFA) 2025, Boao, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

Katika dunia yenye misukosuko ambapo ushuru unazidi kutumiwa kama silaha, "mwelekeo unaoleta wasiwasi umeibuka: biashara duniani inazidi kutegemea nguvu na kulazimisha, badala ya sheria," amesema Waziri Mkuu wa zamani wa Italia na Kamishna wa Uchumi wa Ulaya Paolo Gentiloni.

Daniel Palotai, naibu gavana wa benki kuu ya Hungary Magyar Nemzeti Bank, ameonya kwamba hatua za ushuru zitapotosha na kutenganisha uchumi, na kusababisha madhara ya kudumu kwa miundo ya kiuchumi.

Robert Koopman, mchumi mkuu wa zamani wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), amesema kwamba sera zinazobadilika badilika za ushuru na udhibiti za Marekani zimeongeza hali ya kutokuwa na uhakika katika mazingira ya biashara, na kufanya kuwa vigumu sana kwa kampuni kufanya maamuzi ya muda mrefu na kuandaa mikakati ya maendeleo.

Kutokana na hali hiyo, washiriki wa jukwaa hilo wamekubaliana kwamba kuimarisha ushirikiano na kushikilia mfumo wa pande nyingi ni njia muhimu na zenye ufanisi za kukabiliana na athari mbaya za ushuru na kufufua ukuaji duniani.

"Hakuna nchi inayoweza kubaki ikiwa imejitenga kwenye dunia ya hali ya kutokuwa na uhakika," Wong amesisitiza, akibainisha kuwa ushirikiano wa kuvuka mipaka unabaki kuwa muhimu katikati ya mgawanyiko wa mfumo wa biashara duniani.

Picha hii iliyopigwa Mei 5, 2023 ikionyesha ukumbi wa Maonyesho ya Kwanza ya Kiuchumi na Biashara ya RCEP ya Hunan (Huaihua) katika Mji wa Huaihua, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China. (Xinhua/Yu Chunsheng)

Picha hii iliyopigwa Mei 5, 2023 ikionyesha ukumbi wa Maonyesho ya Kwanza ya Kiuchumi na Biashara ya RCEP ya Hunan (Huaihua) katika Mji wa Huaihua, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China. (Xinhua/Yu Chunsheng)

Jukwaa hilo pia limeshuhudia mijadala mipana kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani, mada inayoonekana sana kuwa ni muhimu kwa utulivu na ustawi wa uchumi duniani.

Li Cheng, profesa katika Idara ya Siasa na Utawala wa Umma ya Chuo Kikuu cha Hong Kong, amesema anatumai kwamba nchi hizo mbili zitaendelea kusonga mbele na kudumisha mazungumzo na kubadilishana.

Amesisitiza kwamba mivutano inayozidi kuongezeka haitumikii maslahi ya mtu yeyote, akiongeza kuwa licha ya tofauti zao, nchi zote mbili zinathamini utulivu wa mambo ya fedha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha